Facebook Comments Box

Sunday, February 10, 2013

MAANDAMANO YA CHADEMA YAPIGWA MARUFUKU

CHADEMA imesema imelazimika kuratibu maandamano na mkutano wa hadhara kama ishara ya kuwapokea wabunge wa upinzani kwa madai ya kuwashitakia Wananchi kitendo cha Bunge kuondoa kwa hoja zao binafsi.

Moja ya h oja hizo ni hoja binafsi ya Mnyika iliyokuwa ikipendekeza Bunge lijadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika jiji la Dar es Salaam, hoja ambayo ilitupiliwa mbali na kuzua mtafaruku bungeni.

Hoja nyingine ni ya Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia aliyoitoa bungeni juu ya udhaifu wa mitaala ya elimu nchini.

Jeshi la Polisi nchini kupitia Kamanda wa Polisi wa mkoa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo amesema ni marufuku kwa CHADEMA kuandamana kama walivyokusudia ila, ni ruhusa kufanya mkutano.

Amesema sababu za kuzuia maandamano hayo ni kutokana na usumbufu utakaojitokeza katika maeneo ambayo maandamano hayo yamepangwa kupitia ikiwa ni pamoja na kuingilia na pengine kuzuia shughuli za kawaida za maeneo hayo, matumizi ya barabara na pengine kuchangia vitendo vya uharibifu wa mali na uvunjifu wa amani. Hivyo akasema alikwishakuwasiliana na viongozi wa CHADEMA wa Temeke kuhusu suala hilo na kuwataarifu kuwa maandamano yoyote yatakayofanyika yatakuwa ni kinyume na sheria na hivyo itawalazimu Polisi kuchukua hatua za kisheria pale inapobidi.

Naye Kamanda wa CHADEMA anayeratibu maandamano hayo, Benson Kigaila alisema maandalizi ya maandamano hayo yanaendelea kama yalivyopangwa kutokana na kuwa hajapokea ujumbe wowote kutoka Jeshi la Polisi kama walivyoahidi kumpigia simu kwa maelezo zaidi.

Maandamano hayo yamepangwa kufanyika kuanzia TAZARA na kuhitimishwa kwa mkutano wa hadhara wilayani Temeke.

Benson alisema mkutano huo ni mwanzo wa mfululizo wa mikutano itakayofanyika kwenye kanda 10 zilizotengwa na CHADEMA, kuanzia mwenzi huu.



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU