Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Muhuga
aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Tanzania katika sherehe za
maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu kuzaliwa kwake.
Mgeni rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta
akiwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo katika
Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa Tanzania kusheherekea
miaka 67 tangu uanzishwe.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimlaki na
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaa leo.
Pichani Juu na Chini ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt.
Alberic Kacou (katikati) akimtambulisha Mh. Samwel Sitta kwa baadhi ya
Wakurugenzi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akipokea heshima ya wimbo
wa Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam leo kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa
baada ya kutimiza miaka 67 ya UN tangu kuanzishwa.
Mh. Samuel Sitta akikagua gwaride maalum katika kilele cha wiki ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa.
Waziri wa Afrika Mashariki akishuhudia upandishwaji wa bendera ya Umoja
wa Mataifa ikiwa ni ishara ya kusheherekea miaka 67 ya Umoja huo katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar leo.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mgeni
rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta na Mkuu
wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meha Jenerali Raphael Muhuga wakiwa
Meza kuu.
Pichani Juu na Chini ni viongozi wa Madhehebu ya Dini nchini wakiomba
Dua kwa ajili ya kubariki sherehe za kutimiza miaka 67 ya Umoja wa
Mataifa tangu kuanzishwa.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akizungumza
katika sherehe za kutimiza miaka 67 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa
Mataifa (UN) katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Sitta
aliipongeza Umoja wa Mataifa kwa kuisaidia Tanzania katika nyanja
mbalimbali za maendeleo ili kutokomeza umaskini.Waziri Sitta alisisitiza
kwamba bado Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto nchini kama vile
amani na usalama, tatizo la njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa
silaha za maangamizi.Mh. Sitta alifafanua katika kilele cha sherehe hizo
umuhimu wa kupitia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo ya
millennia.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akitoa
nasaha zake wakati wa maadhimisho ya umoja huo katika viwanja vya
Karimjee alisema matatizo ya njaa, kupanda kwa bei za mafuta na
mtikisiko wa uchumi duniani ni kati ya changamoto kubwa ambazo Umoja wa
Mataifa inakabiliana navyo katika dunia ya leo. Dtk Kacou pia
aliipongeza Tanzania katika juhudi zake za kupunguza vifo vya wakinamama
wakati wa kujifungua na watoto ili waweze kufikia malengo ya millennia
itakapofika 2015.Mratibu Mkazi wa UN alisema Tanzania imepunguza kwa
kiasi kikubwa maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi.
Katibu wa UNA Tanzania Fancy Nkuhi akizungumza kwenye hafla hiyo
alisema umoja wa mataifa imefanya kazi kubwa katika kuwaunganisha vijana
wa bara la Afrika. Nkuhi alisema kupitia YUNA walitoa elimu ya afya ya
uzazi na ugonjwa wa Ukimwi kwa vijana katika mikoa kumi hapa nchini
Tanzania katika harakati ya kuelimisha vijana madhara ya ugonjwa huo na
afya ya uzazi kwa vijana.
Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa kiingereza ya Heritage (Heritage
English Medium Schools) ambao walikuwa kivutio wakati wa maadhimisho ya
miaka 67 ya wiki ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakiwa katika
gwaride maalum kupamba sherehe hiyo.
Meza kuu ikifurahia jambo wakati wa gwaride la watoto wa shule ya
Heritage baada ya kuonyesha mbwembwe katika kupamba sherehe hiyo.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Azania wakitoa burudani ya Wimbo maalum wa kuipongeza UN kutimiza miaka 67 ya kuzaliwa.
Wanafunzi kutoka shule ya mchepuo wa kiingereza ya Heritage (Heritage
English Medium Schools) wakiimba wimbo maalum uliobeba ujumbe wa
kuhimiza utunzaji wa amani miongoni mwa mataifa wakati wa maadhimisho ya
miaka 67 ya Umoja wa Mataifa.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Mabalozi, Wakurugenzi wa Mashirika ya
Umoja wa Mataifa na Wafanyakazi wa UN na wageni mbalimbali
waliohudhuria sherehe hizo.
Pichani ni baadhi ya maafisa wa Jeshi waliohudhuria sherehe hizo.
Waziri Sitta akiwa ameambatana na Mwenyeji wake Mratibu Mkazi wa UN
Tanzania Dkt. Alberic Kacou (kushoto) wakisikiliza maelezo kutoka kwa
Afisa wa Kitengo cha maafa UN Bw. Mdathiru Abubakar (wa pili kushoto)
akielezea namna ya shirika la Umoja wa Mataifa linavyoshiriki pindi
inapotokea maafa nchini. Kulia ni Judith Bihondwa wa UNICEF.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu (kulia)
akifafanua utendaji wa kazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia
mashirika yake 21 yanavyofanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Tanzania
kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta (wa pili
kushoto) aliyeambata na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt.
Alberic Kacou.
Mwenyekiti wa Shirikisho la vijana la Umoja wa Mataifa nchini (YUNA)
Bw. Lwidiko Edward akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye banda la maonyesho la Umoja wa Mataifa
katika viwanja vya Karimjee jijini Dar.
Waziri Sitta katika banda la maonyesho la shirika linalohudumia
wakimbizi nchini (UNHCR). Katikati ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
nchini Dkt. Alberic Kacou na kushoto ni Afisa Habari kutoka kitengo cha
habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Stella Vuzo.
Afisa Itifaki na Uhusiano wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha
(AICC) Bw. Rodney Thadeus akimweleza Waziri Sitta jinsi ya kituo cha
Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kinavyojipambanua kwa kupokea
wageni mbalimbali wanaofanya mikutano katika kituo hicho na kutmia
mwanya huo kutangaza Utalii na vivutio vya nchi.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta na Mratibu
Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou katika picha ya pamoja na
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye
banda la maonyesho katika wiki ya Umoja wa Mataifa.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog