Facebook Comments Box

Sunday, August 26, 2012

HASHEEM THABEET NA NYOTA WENZAKE WA NBA WATOA MAFUNZO YA KIKAPU DAR






NYOTA wa mpira wa kikapu kutoka Marekani, Hasheem Thabeet Mtanzania anayehezea Oklahoma City, Luol Deng Muingereza mwenye asili ya Sudan Kusini, anayechezea Chicago Bulls leo wameendesha programu ya kliniki kusaka vipaji vya mpira wa kikapu kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Dar es Salaam kwenye viwanja vyta Don Bosco, Upanga.


Kliniki hiyo ilihudhuria na nyota wengine wa NBA, akiwemo Adam Andre, Masai Ujiri, mmiliiki na Meneja wa timu ya Denver Nuggets, Amadaou Gall Fall na Kocha J.


Alikuwepo pia Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo Tanzania, Juliana Yassoda, Balozi Mdogo wa Marekani, Robert K Scott, Rais wa Chama cha Mpira wa Kikapu (TBF), Mussa Mziya na Makamu wake, Phares Magesa.

Zoezi lilianza saa nne asubuhi kwa hotuba ndefu, zilizowafanya watoto waungue juwa muda wa zaidi ya saa mbili, kabla ya kuanza kupewa mafunzo hayo. Pichani ni watoto waliohudhuria wakiteseka na jua kwa kusikiliaza hotuba ndefu.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU