Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kama wanavyo onekana wakiteta jambo Toka kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, wa katikati yao ni Profesa Lipumba wa CUF na mwisho ni Joseph Mbatia wa NCCR.
Viongozi hao wakiwa wameshikana mikono kuonesha kuwa wao ni wamoja.
Baada ya Chama cha mapinduzi CCM kumpata Mgombea wake wa kiti cha urais wiki iliyopita mkoani Dodoma ambae ni John Pombe Joseph Magufuli.
Wanachama wa Umoja wa Katiba ya wananchi (UKAWA) wamekuwa na duku duku la kufahamu mgombea wao atakuwa nani.
Hali hiyo imeleta hamasa sana kwa wanachama hao kiasi cha kuona kama viongozi wao wanachelewa kuwajulisha mgombea wao ni nani na pia kuleta hofu kuwa CUF wamejitoa katika umoja huo.
Lakini CUF kupitia Naibu Katibu Mkuu wao wa Bara Magdalena Sakaya ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazoendelea kuenea, amethibitisha kuwa wao hawaja jitoa Ukawa na kuhusu kutokuwepo kwenye kikao akasema walichelewa kupata taarifa za kikao hicho maana hata wao wana vikao vingi ambapo wanajadili jinsi ambavyo madaraka yatakavyo kuwa endapo wakishinda uchaguzi mkuu huo ambao utafanyika Oktoba.
Naibu Katibu Mkuu wa Cuf Bi Magdalena Sakaya akijibu baadhi ya Tuhuma hizo
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog