Wizara ya Sheria ya Marekani imechapisha taarifa inayoelezea jinsi
Afisa wa zamani wa FIFA Chuck Blazer alivyokiri kuwa yeye pamoja na
wenzake walipokea rushwa ikiwa ni pamoja na kuichagua Afrika Kusini kuwa
mwenyeji wa fainali ya kombe la dunia mwaka 2010.
Katika
taarifa hiyo imeweka wazi mtandao wa malipo ya rushwa ulivyokuwa
ukifanywa ndani ya shirikisho la soka duniani FIFA, taarifa zinazoegemea
uchunguzi uliofanywa na shirika la kijasusi la Marekani FBI.
Taarifa
hiyo ambayo inamwelezea Afisa huyo wa zamani wa Fifa kukiri
kupokea rushwa sasa huenda ikaibua mengi kwenye kashfa ya rushwa
inayoindamana shirikisho la FIFA.
Mmerakani
huyo kwenye taarifa hiyo inadai alikuwa ni mmoja wa watu waliosuka
mipango ya kupokea rushwa katika tukio jingine la fainali la kombe la
dunia 1998.
Taarifa
za Kukiri zipo katika maandishi wakati wa kesi yake mwaka 2013 ilipokuwa akisikilizwa katika mahakama ya Easten New York huko
Marekani ambapo alikiri makosa kumi yaliyokuwa yanamkabili.
Blazer
alikuwa afisa wa ngazi ya juu wa FIFA eneo la kanda ya Amerika Kaskazini na
Kati na ukanda wa nchi Caribbean kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2011.
Marekani
imefungua kesi ya rushwa inayowakabili maafisa wa FIFA jambo lililofanya
Rais wa FIFA Sepp Blatter kuamua kutangaza kujiuzulu.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog