Facebook Comments Box

Sunday, October 26, 2014

SIMBA YAWASIMAMISHA KIEMBA,KISIGA NA CHANONGO

AMRI KIEMBA
Klabu ya Simba SC imewasimamisha wachezaji wake watatu kutokana na kile ninachodhaniwa wachezaji hao kuwa sehemu ya klabu hiyo kufanya vibaya, wachezaji waliosimamishwa ni viungo Amri Kiemba,Shabani Kisiga na Haruna Chanongo,hapo jana jijini Mbeya Simba ililazimishwa sare ya tano msimu huu na Prisons.
Shabaan Kisiga

Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya klabu hiyo kinasema pia benchi la ufundi limepewa changamoto ya kuakikisha timu hiyo inakusanya pointi tisa  kutoka kwenye michezo mitatu inafuata kama ikishindikana basi benchi Zima la ufundi nalo litapigwa chini.

Habari zaidi zikisema kuwa mshambuliaji wa kigeni Hamis Tambwe akipewa onyo kwa kuhusishwa na Simba ukawa huku Ramadhan Singano nae akipewa onyo kali pia.

 Kocha msaidizi Matola na mtoa tiba kwa vitendo Bwana Gembe wamesimamishwa kwa muda usio julikana.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU