Stori: Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete, leo atapokea
‘Katiba Mpya’ inayopendekezwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum,
Samuel Sitta, katika tukio linalotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma.
Rais Jakaya Kikwete
Bunge
hilo maalum, lilihitimisha kazi yake ngumu ya kujadili rasimu ya katiba
mpya iliyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba Oktoba 4 mwaka huu, baada ya Kamati ya
Uandishi chini ya Andrew Chenge kuwa imewasilisha katiba inayopendekezwa
iliyokubaliwa na wajumbe kutoka Bara na Visiwani.
Katiba
hiyo inayopendekezwa, ilipatikana licha ya baadhi ya wajumbe kutoka
vyama vya upinzani kujitoa kwa madai ya kuburuzwa na wenzao wa chama
tawala, kitendo kilichoibua mjadala wa kitaifa huku makundi mbalimbali
yakipingana, wengine wakiwaunga mkono na wengine wakiwapinga.
GPL.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog