Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Maktaba ya Kirais ya Rais Bush (Bush Presidential Library)
na kujionea nafasi kubwa iliyotolewa kwa Tanzania na zawadi ambazo Rais
Bush alizipata katika ziara yake rasmi ya Tanzania wakati akiwa Rais wa
Marekani. Maktaba hiyo ya kuvutia inaendeshwa kwa teknolojia ya kisasa
kabisa ya habari na mawasiliano.
Rais Kikwete alikuwa amesimama mjini Dallas kwa muda akiwa njiani kutoka Washington D.C., kwenda
Houston, jimbo hilo la Texas kuhudhuria mkutano wa wafanyabiashara
wa mafuta na gesi ambao wanataka kuwekeza katika sekta hiyo hapa
Tanzania.
Rais Kikwete amekuwa Marekani kwa ziara ya
kikazi ya siku tisa, ambako miongoni mwa mambo mengine, amehudhuria
Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Marekani na Afrika uliofikia kilele chake
jana kwa kikao kilichoendeshwa na Rais Barack Obama wa Marekani katika
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mjini Washington D.C.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog