SIMBA SC
imetoa sare ya sita mfululizo tangu kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, baada ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa
Jamhuri, Morogoro jioni ya jana.
Hii inakuwa ni mechi ya 12 kwa Simba bila ushindi ukijumlisha na mechi sita za mwisho za msimu uliopita. Swala hili la kutoa suluhu limepelekea Simba kumpa kocha wa Phiri mechi tatu za mwisho na akihitajika kushinda mechi mbili. Jana wametoa suluhu mechi ya kwanza na zimebaki mbili, Hii ina maana akitoa suluhu yoyote au kufungwa ndio utakuwa mwisho wa Kocha huyo ambae ana historia ya kuja Simba na kufundisha mara kwa mara nusu msimu ikifika msimu mwingine anaaga kuwa ana matatizo ya kifamilia na harudi tena.
Suluhu hiyo inawafanya Mtibwa wafikishe pointi 14 kileleni mwa ligi hiyo, wakati Simba SC imefikisha pointi 6 jana.Simba SC
ilikwenda kupumzika ikiwa tayari inaongoza kwa bao 1-0, lililotiwa
kimiani na beki wa kimataifa wa Uganda, Joseph Owino dakika ya 35 kwa
kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Emmanuel Okwi.
Hali hiyo
iliwafanya vinara wa hao wa Ligi Kuu wapate bao la kusawazisha dakika
ya 58, mfungaji Mussa Hassan Mgosi aliyetumia makosa ya beki wa kulia,
William Lucian ‘Gallas’ kuchanganyana na kipa wake, Manyika Jr.
VIKOSI VILIKUWA HIVI:
Mtibwa
Sugar: Said Mohammed, Hassan Ramadhani, David Luhende, Andrew Vincent,
Salim Mbonde, Shaaban Nditi, Mussa Ngosi, Mohamed Ibrahim, Ame Ally,
Mussa Nampaka na Ally Shomary.
Simba
SC: Peter Manyika, William Lucian ‘Gallas’, Mohammed Hussein
‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani
Singano ‘Messi’, Awadh Juma, Elias Maguri/Amisi Tambwe dk76, Said Ndemla
na Emmanuel Okwi/Uhuru Suleiman dk75.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog