KIKOSI CHA TIMU YA SIMBA.
WACHEZAJI WA SIMBA WAKIMSIKILIZA KOCHA WAO PATRICK PHIRI.
KIKOSI CHA TIMU YA YANGA.
WACHEZAJI WA YANGA WAKISHANGILIA MOJA YA BAO LAO.
kitongoni blog:
Mpaka kwenye miaka
ya 90 kulekea mpambano wa
watani wa jadi
kulikuwa na imani
za kishirikiana za mvua zikichukua
nafasi kuliko hivi
sasa, itakumbumbukwa kwamba ilifikia
hatua timu ya
Yanga wanapoona mvua
imenyesha wao walikuwa
wakiingiwa na hofu
zaidi ya kuupoteza mchezo huo
huku upande wa
pili wa Simba nao
wakichekelea kunyesha kwa
mvua wakimaanisha kuwa
lazima wataibuka washindi.
Ama
kwa hakika tukio hilo
lilikuwa lina nafasi
kubwa kwa kuwa
kweli siku ya
mpambano huo kama
mvua haikunyesha Simba
walifungwa au kutoka
sare na pale
iliponyesha mvua tu ni lazima
Yanga wangefungwa.
Lakini
kunako miaka hii ya
2000
mambo sasa yamebadilika
na yeyeto Yule
anaweza kupata ushindi
katika hali yoyote ile liwake
jua ainyeshe mvua,
na hili ndiyo
miongoni mwa mambo
yanayozidi kuupa ladha
mchezo huu kuwa
vigumu kupata utabiri
wa nani mshindi.
Jambo lingine ni
zile kambi zao
ambazo kama Yanga
wakitokea Pemba au
Bagamoyo Mbegani huwa
wana uhakika zaidi
wa kupata ushindi
kuliko kuweka kambi
yao Jijini Dar
es salaam, wakati
Simba wao huwa
wana uhakika zaidi
wa kupata ushindi
kama tu wametokea
Unguja au Dar
es salaam maeneo
ya Bamba Beach.
Katika
mechi hii kambi
za timu zote
hizo hazikuwa kwenye
sehemu zile zilizo zoeleka
na hali hiyo imefanya
kuwa na tambo
nyingi kutoka kwa
mashabiki wake na kila
upande kuamini kuwa
wataibuka washindi.
Jicho la
kitongoni blog litakuwepo kukujuza
kila kitu ambacho
kitatokea ikiwa ni
pamoja na visa na
vibweka vyote vitakavyojiri
uwanja wa Taifa
tarehe 18/10/2014, Jumamosi.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog