Facebook Comments Box

Monday, May 26, 2014

VIONGOZI WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WATIWA MBARONI.

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefanikiwa
kuwakamata viongozi sita wa makundi ya uhalifu maarufu kwa
majina ya Mbwa Mwitu na Panya Road.Akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi wa kanda
hiyo, Suleiman Kova, aliwataja viongozi hao kuwa ni Athumani Said
(20), Joseph Ponela, Clement Petter (25) na Romans Vitus (18)
wakazi wa Kigogo.Wengine ni Mwinshehe Adamu (37) mkazi wa
Temeke na Daniel Petter (25) mkazi wa Yombo, huku kamanda
huyo akibainisha kwamba maeneo yenye vijana hao wahalifu ni
Kigogo,
Magomeni, Tabata, Manzese na Mbagala ambapo askari wa
kutosha wapo kwa lengo la kuwadhibiti. aliwaonya wanaoeneza
uzushi kwamba makundi hayo ya wahalifu yamevamia maeneo
hayo jambo alilodai kuwakosesha wananchi amani huku akisisitiza
kuwa si kweli.Alisema uchunguzi wa jeshi hilo umebaini kwamba
chanzo cha uvumi huo ni baada ya mauaji ya vibaka wawili
walihusishwa na makundi hayo yaliyotokea Mei 18 na Mei 20
mwaka huu eneo la Kigogo Sambusa.
CHANZO:FREEMEDIA


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU