Kikosi cha Yanga |
MABINGWA
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yana SC wameanza vema
kampeni za kutetea taji lao, baada ya kuwafumua Ashanti United ‘Watoto
wa Jiji’ mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao
ya Yanga leo yalifungwa na Jerry Tegete dakika za 10 na 57, Simon Msuva
dakika ya 47, Haruna Niyonzima dakika ya 73 na Nizar Khalfan dakika ya
90, wakati bao pekee la Ashanti lilifungwa na Shaaban Juma dakika ya 89
Young Africans inayonolewa na kocha mholanzi Ernie Brandts imeanza
vizuri harakati zake za kutetea Ubingwa kwa kuhakikisha inashinda mchezo
wa mwanzo na ndivyo vijana wa Jangwani walivyofanya.
Ilimchukua
dakika 10 Jerson Tegete kuipatia Young Africans la kwanza kwa kumchambua
mlinda lango wa Ashanti kufuatia pasi nzuri wa winga wa kulia Saimon
Msuva kuitoka ngome ya Ashanti na kumpasia mfungaji aliyeukwamisha mpira
wavuni bila ajizi.
Ashanti walifanya mashambulizi langoni mwa
Yanga kupitia kwa Hussein Sued lakini ukuta wa Yanga uliokuwa chini ya
Mbuyu Twite na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' ulikuwa kikwazo kwake
kumfikia mlinda mlango Ally Mustapha 'Barthez'.
Kiungo Athuman Idd
'Chuji' alitolewa nje dakika ya 18 ya mchezo kuufuaia kuumia na
kushinda na kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo
Frank Domayo 'Chumvi' .
Kutokua makini kwa washambuliji wa Yanga
Didier Kavumbagu, Saimon Msuva na Jerson Tegete kulizifanya timu kwenda
mapumziko zikwa 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga
kujipatia bao la pili dakika ya 48 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji
Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Ashanti na kuachia shuti kali
liliokwenda moja kwa moja wavuni.
Jerson Tegete aliipatia Young
Africans bao tatu dakika ya 58 kwa usatdi wa hali ya juu akimalizia pasi
safi ya Saimon Msubva aliyewatoka walinzi wa Ashanti United na kujaza
krosi safi ambayo Tegete aliiweka kifuani kabla ya kumchambua mlinda
mlango.
Yanga iliendelea kucheza inavyotaka huku ikitawala dimba
la katikati kupitia kwa viungo wake Haruna Niyonzima, Salum Telela na
Frank Domayo hali iliyowapelekea wachezaji wa Ashanti kucheza faulo
nyingi na mwamuzi kuwaadhibu kwa kadi za njano na mmoja wao kutolewa nje
kwa kadi nyekundu.
Haruna Niyonzima aliipatia Young Africans bao
la nne dakika ya 74 ya mchezo kwa kichwa, akimalizia mpira wa adhabu
uliopigwa na mlinzi wa pembeni David Luhende kufuatia Saimon Msuva
aliyekuwa amechezewa madhambi na walinzi wa Ashanti United.
Dakika
ya 90 Ashanti United walijipatia bao kupitia kwa Shaban Juma kufuatia
uzembe wa walinzi wa Yanga waliotegeana kumkaba mfungaji aliyeukokota
mpira toka nje ya 18 na kuingia nao ndani ya sita na kumfunga mlinda
mlango Ally Mustapha 'Barthez'.
Huku washabiki na wapenzi wa soka
wakiwa wanatoka nje wakijua mpira umemalizika, Nizar Khalfani aliipatia
Young Africans bao la tano na kukamilisha ushindi huo mnono akimalizia
pasi ya Saimon Msuva ambaye leo alikua mwiba mkali kwa walinzi wa
Ashanti.
Mpaka dakika 90 za mchezo za mwamuzi Israel Mjuni Nkongo zinamalizika, Young Africans 5 -1 Coastal Union.
Kocha
mkuu wa Yanga Ernie Brandts amekipongeza kikosi chake na kusema ni
mwanzo mzuri katika msimu huu, aidha amesema wachezaji wake wangekuwa
makini basi leo wangeibuka na ushindi mnono zaidi ya hizo bao tano
walizozipata kutoka kwa wauza mitumba wa Ilala - Ashanti united.
Mara
baada ya mchezo wa leo wachezaji wote wamepewa mapumziko siku ya kesho
mpaka siku ya jumatatu watakapoanza mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya
Coastal Union ya Tanga siku ya jumatano tarehe 28.08.2013 katika dimba
la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans: 1.Ally
Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub
'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji'/Frank Domayo,
7.Saimon Msuva, 8.Salum Telela, 9.Didier Kavumbagu/Hussein Javu,
10.Jerson Tegete/Nizar Khalfani, 11.Haruna Niyonzima
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog