Tutapambana hadi kieleweke; Bin Kleb kushoto akikumbatiana na Ngassa baada ya kusaini Yanga SC. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yana SC, Mussa Katabaro |
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Abdallah Ahmed Bin Kleb amesema jana jioni kwamba, mawakili wao watatu leo wamewasilisha Rufaa hiyo TFF ikiwa imebeba hoja nzito, ambazo wanaamini zitatosha kumkomboa Ngassa.
“Mawakili wetu nadhani watakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia Rufaa waliyowasilisha, kwa kweli katika hili suala mchezaji hajatendewa haki, nasi tunawajibika kumsaidia,”alisema Bin Kleb.
Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa ilibaini kuwa Ngassa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.
Kamati hiyo pia ilimfungia mechi sita za mashindano na kumtaka awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo na akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.
Ngassa alisaini Yanga baada ya kuitumikia Simba SC kwa mwaka mmoja akitokea Azam FC, akiwaambia viongozi wa Jangwani amemaliza Mkataba wake Msimbazi.
Lakini baadaye Simba SC ikaibua Mkataba iliyosaini na Ngassa na inaonyesha anatakiwa kufanya kazi Msimbazi kwa mwaka mmoja mwingine.
TFF nayo ikathibitisha, inao Mkataba ambao Ngassa alisani na Simba SC.
Hoja kuu ya Yanga katika Rufaa yao ni kitendo cha Simba SC kumsainisha Ngassa Mkataba wakati imemchukua kwa mkopo kutoka na Azam na bado alikuwa ana Mkataba na klabu hiyo- na kwa kuwa wanaamini hilo ni kosa kwa mujibu wa kanuni, wanapingana na adhabu alizopewa.
CHANZO: BIN ZUBEIRY
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog