
Dar es Salaam/Moro. Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu 
Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda yupo chini ya ulinzi huku akitibiwa 
majeraha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Sheikh Ponda alisafirishwa usiku wa manane kutoka 
Morogoro baada ya juzi kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni mtutu wa 
bomu saa 12:25 jioni alipokuwa akisindikizwa na wafuasi wake kwenda 
katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mara baada ya kumaliza kutoa 
mhadhara katika kongamano mjini hapo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema, alidai kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi tatu begani.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya Ponda zilisema 
kwamba baada ya kupata taarifa za kupigwa risasi, baadhi ya masheikh 
walifunga safari kwenda Morogoro na kumrejesha Dar es Salaam usiku 
huohuo. Kabla ya kurudishwa Dar es Salaam, imeelezwa kuwa Sheikh Ponda 
alipelekwa katika Zahanati ya Islamic Foundation.
Mmoja wa wanafamilia alidokeza kwamba Sheikh Ponda
 alifichwa na alikuwa chini ya ulinzi mkali wa wafuasi wake na hakuna 
aliyeruhusiwa kumsogelea.
Muhimbili
Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye jana 
zilisema kuwa alifikishwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya 
kupatiwa matibabu.
Sheikh Ponda alifikishwa Muhimbili jana saa 7:18 
mchana na alipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa wa dharura na baadaye 
alitolewa na kupelekwa kwenye chumba cha x-ray kwa ajili ya vipimo. 
Baadaye alipelekwa chumba cha upasuaji.
Eneo kubwa la hospitali hiyo lilikuwa na idadi 
kubwa ya askari na mmoja wa askari waliokuwa doria hospitalini hapo 
alisema walitawanywa kwenye hospitali mbalimbali za Dar es Salaam baada 
ya kupata taarifa kuwa angeletwa kwa matibabu.
“Nakuambia tuko hapa tangu saa kumi na moja 
asubuhi, tumetawanywa hospitali mbalimbali baada ya kupata taarifa kuwa 
analetwa Dar. Bahati nzuri kaletwa hapa Muhimbili... tunasubiri apate 
matibabu na tutamtia mbaroni,” alisema askari huyo.
Taarifa ya polisi
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema jana 
katika taarifa yake kuwa Sheikh Ponda yuko Hospitali ya Muhimbili 
akitibiwa baada ya kupata majeraha yaliyotokana na purukushani na polisi
 wakati wafuasi wake walipokuwa wanataka kumtorosha
 
SOURSE:MWANANCHI  
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog