Kikosi cha Yanga ambao ndio mabingwa wa Tanzania Bara |
Dar es Salaam.Siri ya Yanga kugomea mkataba wa udhamini wa Azam
TV, inadaiwa ni kutokana na klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani kuwa na
mazungumzo na Kampuni ya Zuku TV kwa ajili ya kuonyesha kipindi cha
Yanga.
Habari za uhakika ambazo Mwananchi imezipata
kutoka kwa kiongozi mmoja wa Kamati ya Utendaji ya Yanga zinasema kuwa
Zuku wapo tayari kutoa Sh 400 milioni kudhamini kipindi cha Yanga ‘Yanga
TV Show’.
“Mazungumzo ya awali yalikuwa na ofa ya Sh 300
milioni, sasa wamekuja na ofa ya Sh 400 milioni ndiyo ipo mezani,
mazungumzo yanaendelea,”kilisema chanzo hicho.
Iwapo watakubaliana, mashabiki wa Yanga watapata
fursa ya kuona programu za mazoezi ya timu yao, mahojiano ya wachezaji,
makocha, viongozi na masuala mbalimbali ya maendeleo ya klabu ya Yanga.
Chanzo hicho
kimedai kuwa mazungumzo hayo ya chini kwa chini yanayoendelea baina ya Yanga na Zuku ndiyo yanasababisha klabu hiyo ya Jangwani kukataa ofa ya Azam ambayo hivi karibuni iliiingia mkataba na Simba wenye thamani ya Sh 331 milioni kwa muda wa miaka mitatu huku Yanga wakikalia kimya ofa yao.
kimedai kuwa mazungumzo hayo ya chini kwa chini yanayoendelea baina ya Yanga na Zuku ndiyo yanasababisha klabu hiyo ya Jangwani kukataa ofa ya Azam ambayo hivi karibuni iliiingia mkataba na Simba wenye thamani ya Sh 331 milioni kwa muda wa miaka mitatu huku Yanga wakikalia kimya ofa yao.
Hata hivyo msemaji wa Zuku, Julie Kalanje
alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema kwa kifupi, “Kuna mambo mengi,
lakini kwa sasa mwenye haki za TV ni Azam, hakuna mazungumzo yoyote
yanayoendelea na Yanga ila muda muafaka ukifika kuzungumzia jambo hilo
tutawaambia.”
Naye Katibu wa Yanga, Lawrance Mwalusako alisema hakuwapo kwenye mkutano wa majadiliano na Zuku.
“Sijui lolote, ila wewe taarifa hizi umezipata
wapi? Nnaomba uniambie nani aliyekuambia,” alihoji Mwalusako kabla ya
kukata simu.
Madai mengine ya Yanga kukataa mkataba wa udhamini
wa Azam TV, ni kipengele cha CD za mchezo ambazo Azam watazimiliki,
ambapo Yanga watakapozihitaji hawatapewa, pia suala la udini ambalo
wanadai Azam walishawahi kugomea kushiriki michuano ya Tusker kwa kile
walichoeleza yamedhaminiwa na kampuni ya pombe, ambapo hivi sasa Yanga
inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace
Karia akizungumzia suala hilo alisema madai hayo ya Yanga hayana mashiko
kwani klabu zote zitapewa CD za kila mchezo na pia suala la TBL
kuidhamini Yanga siyo peke yao ambao wanadhaminiwa na TBL kwani hata
Simba nao wadhaminiwa na TBL na tayari wameishakubaliana na Azam TV.
“Kwanza mpaka sasa hatujasaini mkataba wowote,
kilichopo mezani ni mkataba wa maelewano vikao vyote kwa upande wa Yanga
wameshiriki Mwalusako (katibu) na Sanga (Makamu) sasa tunashangaa
wanasema hawajashirikishwa,”alisema Karia.
hiyo kwa kumtaka Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kuingilia kati na kukaa mezani na
viongozi wa Yanga ili wamalizane kwa njia ya amani.
Katika mkutano huo uoliudhuriwa na Katibu wa nzima kwa kuhamasisha wanachama wao kugomea mkataba huo.
“Hatuko tayari Azam kudhamini au kuonyesha mechi
zetu, viongozi hawajakurupuka ila taratibu za kumpata Azam hazikufuatwa,
Yanga siyo mamluki, TFF kuna watu wanaendesha mambo kwa maslahi yao
binafsi.
“Viongozi wanadhalilishwa eti hawana uzoefu, klabu
yetu namba moja kwa mapato, leo tunashikiwa mapanga lazima Azam
waonyeshe Subhead andika hapa , andika hapa,andika hapa Subhead andika
hapa andika, andika hapa, subhead andika hapa, andika hapa,
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog