Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw.Jeff Shrader akitoa shukrani zake kwa uongozi na wafanyakazi wa TTCL alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo.Afisa
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akiwashukuru
wawakilishi kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa kutambua mchango
wa TTCL katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani
alipotembelea Nchini Tanzania.
Uongozi wa TTCL pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini katika picha ya pamoja.
Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dtk. Kamugisha Kazaura akibadilishana mawazo na Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Kampuni
ya simu Tanzania (TTCL) imepongezwa na Ubalozi wa Marekani kwa huduma
bora iliyotoa wakati wa ujio wa Rais wa Marekani hapa nchini.
Akitoa
shukrani hizo Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa
nchini Bw. Jeff Shrader amesema, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania
umejipatia sifa kubwa kwa huduma bora na za uhakika kutoka TTCL wakati
wote wa ujio na uwepo wa Rais wa Marekeni hapa nchini.
Ameongeza
kuwa huduma walizozipata zimethibitishwa na taarifa kutoka ofisi
inayoratibu safari za Rais wa Marekani kuwa katika nchi walizopita
Afrika huduma ya mawasiliano ialiyoipata Tanzania ilikuwa ni ya kiwango
cha juu na aliipongeza TTCL na kusema hii ni sifa kubwa kwa Serikali ya
Tanzania na Ubalozi wa Marekani hapa nchini.
Katika
Shukurani zake Bw. Jeff Shrader alioa pia zawadi kwa Afisa Mtendaji
Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura na kwa baadhi ya wawakilishi kutoa
fani mbalimbali za Ufundi na Biashara kwa niaba ya wafanyakazi wote wa
TTCL kama ishara yao ya shukurani kwa TTCL na Taifa kwa ujumla.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog