Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wana
lambalamba Azam fc wanatarajiwa kuondoka Agosti 2 mwaka huu kuelekea
nchini Afrika kusini kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na michuano
ya ligi kuu soka Tanzania bara na michuano ya kimataifa mwakani ambapo
watakaa kwa wiki mbili.
Afisa
habari wa klabu hiyo, Jafar Idd Maganga amesema wameamua kufanya ziara
bondeni kwani wao wameendelea zaidi kisoka kwa maana ya kuwa na ligi
bora, timu bora na mfumo wa kisasa wa kuendesha soka, hivyo watajifunza
mambo mengi kutoka kwao.
Jafar
alisema ziara hiyo itakuwa na manufaa makubwa sana kwani watacheza na
klabu kubwa za huko wakiwemo Supersport United na Orland Pirates.
“Malengo
yetu ni kufanya makubwa katika michuano ya kimataifa, lakini Ubingwa wa
ligi kuu ni muhimu sana kwetu. Na ndio maana tunaenda Afrika kusini
kuweka kambi ya wiki mbili”. Alisema Jafar.
Kuhusu
usajili, Jafar alisema wao hawajasajili mchezaji yeyote mpaka sasa na
hawana mpango wa kufanya hivyo kwani kikosi chao kipo kamili gado.
“Timu
yetu ni nzuri sana, kusajili mara kwa mara kunaharibu timu, sisi tuna
wachezaji wengi wakiwemo vijana wetu na ndio maana hatuhangaiki na
usajili”. Alisema Jafar.
Wakati
huo huo shirikisho la soka Tanzania, TFF, limethibitsha kupokea barua
kutoka klabu ya Azam fc kuwa wanatarajia kuondoka nchini kuelekea Afrika
kusini.
Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema Azam wamefanya vziuri kuwataarifu wao ili waende kwa kibali sahihi.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog