Siku
chache baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Pappis Demba Cisse
kutoa kauli yakugoma kuvaa nembo ya kampuni ya Wonga ambayo hutoa
mikopo yenye riba , mchezaji wa pili ametoka na kuungana na Cisse kwenye
msimamo huo wa kutovaa logo ya Wonga kwa kuwa kampuni hiyo inafanya
biashara ambayo kwa mujibu wa misingi ya dini ya kiislamu ni Haramu.
Kiungo wa Ivory Coast ambaye atakuwepo uwanjani siku ya jumapili
kucheza dhidi ya Taifa Stars Ismael Cheikh Tiote amesema kuwa atazungmza
na wanasheria wake kuangalia wa kutoivaa nembo hiyo . Tiotte kama
ilivyo kwa Cisse ni muislamu anayefuata misingi yote ya dini hiyo na kwa
mujibu wa sheria za dini yake riba kwenye mkopo unaotolewa kwa mtu
mwingine ni haramu.
Newcastle United imesaini mkataba wa miaka minne na kampuni ya Wonga
mkataba ambao umeifanya klabu hiyo kuingia kwenye utata na wachezaji
wenye imani ya dini ya kiislamu . Newcastle United ina wachezaji
wasiopungua watano ambao wamezungmzia kutokuwa tayari kuvaa nembo ya
Wonga jambo linaweza kusababisha klabu hiyo kulazimika kuwauza wachezaji
kama Pappis Cisse , Tiotte na wenzao kwani hawako tayari kutumiwa
kwenye kampeni za matangazo ya kampuni hiyo.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog