Facebook Comments Box

Sunday, June 16, 2013

BAADA YA TUKIO LA BOMU UCHAGUZI WA AHIRISHWA ARUSHA


Kufuatia tukio la mlipuko jana jumamosi Arusha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeahirisha chaguzi za madiwani katika kata zote nne (4) jijini arusha hadi jumapili ya tar 30/6/2013.

 Tume ya taifa ya Uchaguzi imesimamisha kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa udiwani ktk kata nne jijini Arusha. Akizungumza kwa njia ya simu na Radio TBC FM,kutoka Zanzibari mwenyekiti huyo wa tume ya uchaguzi alisema kua wameamua kusimamisha uchaguzi huo ili kuwapa nafasi vyombo vya usalama kuchunguza swala hilo.
Alisema kua sheria inawapa mamlaka kufanya hivyo pale wanapogundua kuwa hakutakua na uhuru wa mpiga kura kwenda kupiga kura. Alisema haiwezekani uchaguzi ufanyike ktk hali kama hiyo huku kukiwa na wasiwasi.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU