Imeandikwa Francis Godwin, Iringa, via blog
WAKATI
maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yalifanyika siku ya Mei
Mosi ikiwa ni pamoja na kuwazawadia wafanyakazi bora, hali ya mambo
katika mkoa wa Iringa ilikuwa tofauti baada mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Iringa Dk Leticia Warioba kudanganywa na baadhi ya waajiri
kutoa zawadi hewa kwa wafanyakazi bora.
Mwandishi alifanya uchunguzi juu ya zawadi wanazopewa wafanyakazi bora kama ni zawadi halisi ama mkopo baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi bora waliotangazwa miaka ya nyuma kudai kuwa kuwa baadhi ya waajiri wamekuwa wakitafuta sifa katika sherehe hizo kwa kuwatangaza wafanyakazi bora bila ya kuwapa zawadi zao.
Aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kaimu mkuu wa mkoa wa Iringa, Dk Warioba alipoulizwa kuhusu lawama za udanganyifu huo alikiri kukabidhi bahasha ambazo baadhi zilikuwa zimeandikwa fedha nyingi ila bado zilikuwa nyepesi zaidi kama ndani hakuna kitu chochote.
"Kweli mimi sikuweza kuzifungua bahasha hizo ila ulichoniuliza ni kweli kabisa bahasha nyingine zilikuwa hazionyeshi kama zina kitu ndani. Mimi napongeza uchunguzi wako ulioufanya utatusaidia kuwabana viongozi wa wawafanyakazi ili kufuatilia hilo"
Awali baadhi ya wafanyakazi bora waliotangazwa mwaka jana walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa fedha zao kama wafanyakazi bora mwaka jana na juzi hadi leo bado hawajalipwa zaidi ya kupewa vyeti na baadhi kulipwa fedha nusu; Hivyo kutaka Serikali ya mkoa wa Iringa kusimamia ahadi yake iliyotolewa na aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kepteni Mstaafu Asser Msangi (ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe) wa kuzifungua bahasha za wafanyakazi bora na kuhakikisha wanapewa fedha zao taslimu badala ya kukopwa.
Kabla ya maadhimisho hayo jitihada za kumsaka mratibu wa maadhimisho hayo ili kujua kama wamefanya utaratibu wa kuchunguza zawadi za wafanyakazi bora zimefanyika ama la, kamati ya maadhimisho hayo chini ya mratibu wake Bw Deus Magesa ilieleza kulifanyia kazi suala hilo na kusema kuwa kila bahasha ya mfanyakazi atakayetangazwa kuwa Mfanyakazi Bora itafunguliwa. Ahadi hiyo halikutekelezwa.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi (TUICO) mkoa wa Iringa, Thomas Mashaka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Mkoa wa Iringa alisema kuwa mbali ya kuwabana waajiri ila ni kweli baadhi yao wamekabidhi ahadi na sio zawadi zilizotangazwa.
Mashaka alitoa muda wa siku tatu kwa waajiri wote waliotoa ahadi hewa kuhakikisha wanatimiza ahadi hizo kwa kuwapa zawadi zao waliotangazwa kuwa ni Wafanyakazi Bora.
"Ni kweli ndugu mwandishi wa habari baadhi ya watu wametoa zawadi hewa hawakutoa hundi wala pesa taslimu kama walivyoandika katika bahasha... ila wapo walioahidi radio pia hawakuweza kuzileta radio pale ila tulipowauliza walidai maandalizi... sasa sisi kama chama tutafuatilia kuona wahusika wamepewa zawadi zao. Hadi Jumamosi kila kitu kitakuwa sawa," alisema Mashaka.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog