Release No. 026
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 12, 2013
WASHABIKI WAZIUNGE MKONO AZAM, SIMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linawaka washabiki wa mpira wamiguu kujitokeza kwa wingi
wikiendi hii kuzishangilia timu za Azam na Simbazitakazocheza mechi za
mashindano ya Afrika jijini Dar es Salaam.Nguvu ya washabiki ni muhimu katika
kuziweza timu hizo kufanya vizuri katikamechi hizo za nyumbani dhidi ya Al
Nasir Juba ya Sudan Kusini na Club Liboloya Angola.Azam itacheza Jumamosi (Februari
16 mwaka huu) dhidi ya Al Nasir katikamechi ya Kombe la Shirikisho wakati Simba
itaikabili Club Libolo kwenyemechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayofanyika
Jumapili. Mechi zotezitachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
LYON, YANGA KUUMANA UWANJA WA TAIFA
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara inamalizaraundi ya 16 kesho (Februari 13 mwaka huu)
kwa mechi kati ya wenyejiAfrican Lyon dhidi ya Yanga itakayochezwa Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.Mechi hiyo itakayochezshwa na mwamuzi Martin Saanya kutoka
Morogoroinakutanisha timu zenye mazingira tofauti. Wakati Yanga wakiwa ndiyo
vinarawa ligi hiyo kwa pointi 33, African Lyon ambayo sasa inanolewa na
SalumBausi inakamata mkia ikiwa na pointi tisa tu.Nayo Toto Africans
itaikaribisha Polisi ya Morogoro kwenye Uwanja wa CCMKirumba jijini Mwanza
katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi JacobAdongo kutoka Musoma. Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga wenye uwezo wakuchukua watazamaji 20,000 utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya MgamboShooting na Oljoro JKT.Nahodha wa zamani wa
Taifa Stars, Mecky Maxime ambaye sasa ni kocha waMtibwa Sugar ataiongoza timu
yake hiyo katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Manungu ulioko
Turiani, Morogoro. Ni kwenye uwanja huo ambapo Mtibwa Sugar katika mechi yao
iliyopita walichapwa mabao 4-1na Azam.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog