Facebook Comments Box

Saturday, August 3, 2013

YANGA YAMUONGEZA HAMISI FRIDAY KIIZA MKATABA WA MIAKA MIWILI

Young Africans Sports Club jana usiku imemuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji Hamis Friday Kiiza kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo.

Kiiza awali mkataba wake ulimalizika mwishoni mwa mwezi mei mwaka huu kabla ya jana kukutana na viongozi wa klabu ya Yanga na kukubaliana kuongeza mkataba huo.

Kiiza anakua ni mchezaji wa nne wa kimataifa atayeitumikia klabu ya Yanga akiwa pamoja na Didier Kavumbagu, Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima.
Ni Majemedari watatu wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC inayohusika pia na masuala ya usajili, Mwenyekiti Abdallah Bin Kleb na Wajumbe wake, Isaac Chanji na Mussa Katabaro wamemaliza kazi hiyo usiku huu.
Zoezi lilifanya katika eneo la bwawa la kuogelea kwenye hoteli ya Protea, Dar es Salaam na Kiiza Jumapili atavaa tena jezi ya Yanga kuichezea kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa.  
Hamis Friday Kiiza "mabao"
 


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU