Facebook Comments Box

Thursday, August 8, 2013

SALAAM ZA IDD AL-FITWR

Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLLaah wa Barakaatuh,
Tunapenda kuwaarifu kuonekana kwa mwezi mpya wa Shawwaal leo hii Jumatano (07 Agusti 2013M). Kwa hiyo, kesho Alkhamiys In Shaa Allaah ni tarehe 1 Shawwaal 1434H (08 Agusti 2013M) na ndio Siku kuu yetu ya ‘Iydul-Fitwr.
Kwa Munaasabah huu wa ‘Iyd Al-Fitwr tunapenda kuchukua fursa hii kuwasilisha salaam zetu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie 'amali zetu na zenu ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNAA WA MINKUM’ (Hivi ndivyo Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi wanapokutana katika siku ya 'Iyd). Na tunamuomba Yeye Aliyetukuka na Mweza, Awajaalie furaha, amani, mapenzi, siha na Iymaan pamoja na karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu.
Mwisho, bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu Waislam wote waliopo kwenye dhiki, vita, ukandamizwaji, njaa, maradhi na wanaodhulumiwa pote duniani. Tukimuomba Allaah (Subhaanahu wa ‘Ta’ala) Awakwamue na kuwapa faraja na nusra.
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutakabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn
Tafadhali bonyeza kwenye picha ifuatayo upate Takbiyrah ya 'Iyd
 
 


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU