Saturday, August 31, 2013
PICHA: FRANSIS CHEKA AKIMCHAKAZA MMAREKANI
 Mgeni
 Rasmi katika Mpambano wa Kimataifa wa kuwani Mkanda wa Ubingwa wa Dunia
 wa WBU,kati ya Mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phil Williams wa 
Marekani,Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella 
Mukangala (mwenye koti jeupe) akimvisha Mkanda wa Ubingwa huo,Bondia 
Francis Cheka baada ya kumshinda kwa Point Mpinzani wake,katika Mchezo 
uliomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es 
Salaam.Kulia ni Bingwa wa Zamani wa Masumbwi,Fransous Bhotha.
 Bondia
 Francis Cheka wa Tanzania (kushoto) akimrushia makonde makali mpinzani 
wake,Phil Williams kutoka nchini Marekani wakati wa mpambano wao wa 
Kimataifa kuwania Mkanda wa Ubingwa wa Dunia wa WBU,uliofanyika usiku 
huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Bondia Francis
 Cheka ameibuka kidedea baada ya kumchapa mpinzani wake huyo kwa Point.
Bondia
 Phil Williams kutoka nchini Marekani (kulia) nae alikuwa akijibu 
mashambulizi kwa mpinzani wake,Francis Cheka.hadi mwisho wa mchezo 
uliokuwa wa raundi 12,Francis Cheka aliweza kuibuka Kidedea kwa kumchapa
 mpinzani wake huyo kwa point na kufanikiwa kumnyang’anya mkanda wa 
Ubingwa wa Dunia wa WBU.
 Chukua hiyoooooo…
 Hapa lazima ukae,mie ndio kisiki cha mpingo:hivyo ndivyo Bondia Francis Cheka alivyoonekana kuifanya kazi yake vilivyo.
 Refa
 wa Mchezo huo akimzuia Bondia Francis Cheka baada ya kumkoleza makonde 
kisawasawa mpinzani wake,yaliyompelekea kwenda chini.
Mpambano ukiendelea.
![]()  | 
| Wanahabari wakipata taswira za mpambano huo. | 
Friday, August 30, 2013
MASAA NANE YATUMIKA KUTENGANISHA MAPACHA MUHIMBILI

Jopo la 
Madaktari Bingwa Saba wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na 
Taasisi ya Mifupa ya hospitali hiyo (Moi), wamefanikiwa kuwatenganisha 
pacha waliokuwa wameungana kiwiliwili.Iliwalazimu mabingwa hao kutumia 
saa nne kufanikisha upasuaji huo. Mmoja wa watoto hao waliotenganishwa, 
amelazwa kwenye Wodi ya Uangalizi Maalumu (ICU) Taasisi ya Mifupa Moi 
wakati kiwiliwili kingine kilifariki.
Jopo la madaktari waliofanikisha 
upasuaji huo ni; bingwa mstaafu wa watoto ambaye aliitwa maalumu kwa 
kazi hiyo, Petronila Ngiloi, Dk Robert Mhina (mifupa) na Profesa Karim 
Manji aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mapigo ya moyo.
 
Wengine ni Dk Karima Khalid aliyekuwa 
akiratibu dawa ya usingizi, Dk Hamis Shaaban (ubongo na uti wa mgongo), 
Dk Zaitun Bokhary (bingwa upasuaji watoto) na Dk Nyangasa (moyo na 
mishipa ya fahamu).
 
Akizungumza baada ya upasuaji huo, Dk 
Shaaban alisema walimfanyia vipimo mtoto ambaye hakuwa amekamilika na 
kugundulika kuwa hakuwa amekamilika viungo vyote achilia mbali kutokuwa 
na kichwa na macho pia hakuwa na moyo, figo, tumbo, maini ila alikuwa na
 uti wa mgongo.
 
"Uti wa mgongo ulikuwepo na ndio 
uliokuwa umeshikana na mwenzake na kuna mshipa mmoja wa fahamu ulikuwa 
unafanya kazi ndio maana alikuwa ukimgusa anachezesha mguu."
 
Alisema kinachoratibiwa kwa sasa ni 
kuangalia dawa ya usingizi aliyopewa mtoto ambaye anaendelea kupumua na 
kwamba ndani ya saa 24, dawa ya usingizi waliyomuwekea mtoto huyo 
itakuwa imeisha na ataanza kunyonya kama kawaida.
Upasuaji
 
Upasuaji
Kazi ya upasuaji huo ilianza saa mbili
 asubuhi kwa mtoto huyo wa jinsi ya kike aliyetimia kuchukuliwa vipimo 
mbalimbali ikiwemo CT Scan, MRI, Ultra sound na vingine vingi kabla ya 
upasuaji kamili kuanza saa tano asubuhi.
 
Dk Shaaban alisema ni mara ya kwanza 
kwa Moi kufanya upasuaji wa aina ile na kwamba mara nyingi wamekuwa 
wakifanya upasuaji wa watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa pamoja na 
mgongo wazi ambao tatizo hilo linasababishwa na upungufu wa madini ya 
folic acid.
 
Kabla ya upasuaji kuanza, mama wa 
mtoto huyo Pili Hija (24) alitumia muda wa nusu saa kufanya maombi 
maalumu ya kumwombea mtoto wake kisha kuwaruhusu madaktari kuendelea na 
upasuaji huo.
 
Akizungumza muda mfupi baada ya 
kuruhusiwa kumwona mtoto wake, Hija alisema: "Ninamshukuru Mungu kwa 
yote na nazidi kumwomba amjalie mwanangu apone kabisa, nawashukuru na 
nitazidi kuwaombea madaktari wanaomtibu mwanangu."Alijifungulia nyumbani
 Agosti 18 maeneo ya Jang'ombe, Zanzibar watoto pacha walioungana mmoja 
akiwa amekamilika viungo vyote na mwingine akiwa na kiwiliwili.
PICHA: DIAMOND AZINDUA VIDEO YAKE NA KUMPA MZEE GURUMO GARI
![]()  | 
| 
 
Mwanamuziki Diamond Platnum akimkabidhi funguo ya gari
aina ya Toyota Funcargo mwanamuziki mkongwe nchini mzee Muhidin Gurumo kama
zawadi yake kwa mkongwe huyo wa muziki baada ya kustaafu rasmi kuimba muziki,
Diamond alitoa zawadi hiyo kwa Gurumo katika hafla yake ya uzinduzi wa video
yake mpya ya wimbo Nomber One aliyoirekodi huko Afrika Kusini ikigharimu kiasi
cha dola elfu 30.000 zaidi ya milioni arobaini za Tanzania, Video hiyo
imetengenezwa kwa viwango vya kimataifa na itaweza kumtangaza vyema kijana huyo
wa kitanzania katika ulimwengu wa muziki hasa kimataifa, Hafla hiyo imefanyika
kwenye hoteli ya Serena Dar es salaam na imehudhuriwa na wasanii pamoja na
waigizaji wa filamu na watu maarufu mbalimbali 
 | 
![]()  | 
| 
 
Mzee  Muhidin Gurumo akimshukuru Diamond kwa
kumzawadia gari jambo ambalo kwake ni kama ndoto kwakuwa amestaafu akiwa hana
usafiri “Yaani sijui hata mke wangu nikimwambia atanielewaje manake ni jambo la
kushangaza kwangu” Alisema mzee Gurumo 
 | 
![]()  | 
| 
 
Diamond akimuongoza mzee Gurumo kwenda kumuonyesha gari 
 | 
![]()  | 
| 
 
Diamond akimuonesha Mzee Gurumo gari 
 | 
![]()  | 
| 
 
Diamond akizungumza machache kushukuru mashabiki wake na
watu mbalimbali waliomsaidia kufikia hapo alipo 
 | 
   ![]()  | 
| 
 
Diamond na madansa wake wakitumbuiza katika hafla hiyo 
 | 
![]()  | 
| 
 
Wasanii mbalimbali pamoja na MaDJ walikuwepo katika hafla
hiyo hapa ni Dully Sykes na MawanaFA wakiwa na baadhi ya MaDJ 
 | 
![]()  | 
| 
 
Maurice Njowoka kutoka Cocacola wa pili kutoka kushoto na
Mwanamuziki AY wa tatu kutoka kushoto pamoja na wadau wengine 
 | 
![]()  | 
| 
 
Mwigizaji Jaquiline Wolper naye alitia timu 
 | 
![]()  | 
| 
 
Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka akiwa na mama yake Diamond 
 | 
![]()  | 
| 
 
Wadau mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo 
 | 
![]()  | 
| 
 
Mzee Gurumo akihojiwa na waandishi wa habari 
 | 
![]()  | 
| 
 
Hawa marafiki zangu wakakumbushia miaka kadhaa
waliyofunga ndoa kwa kulishana mishikaki ilipendeza katikati ni Nancy Sumari
akishuhudia 
 | 
![]()  | 
| 
 
Kulia ni Irene Uwoya kushoto Salma Msangi 
 | 
![]()  | 
| 
 
Kushoto AY na Salama Jabir wakipiga story na wadau
mbalimbali 
 | 
![]()  | 
| 
 
Kutoka kulia ni Raymond Kigosi, Irene Uwoya na JB wakiwa
katika hafla hiyo. 
 | 
      
 
Subscribe to:
Comments (Atom)























