PICHA CHINI NI ZA JANA KATIKA UJIO WAKE
Maofisa
Usalama wa Marekani, wakiingia Uwanja wa Ndgege wa Zamani, jijini Dar es
Salaam, ilikotua ndege ya Rais Barrack Obama wa Marekani kwa ajili ya
kuimarisha ulinzi uwanjani hapo jana. (Picha zote na Kassim
Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Ngoma ya Matarumbeta ya kikundi cha Usambara Group, kikitumbuiza
katika mapokezi ya Rais Obama wa Marekani, aliyewasili jana nchini kwa
ziara ya siku mbili.
Maofisa Usalama wa Marekani, wakiwa juu ya paa la Uwanja wa Ndgege wa
Zamani, jijini Dar es Salaam, ilikotua ndege ya Rais Barrack Obama wa
Marekani kwa ajili ya kuimarisha ulinzi uwanjani hapojana.
Rais Jakaya Kikwete, akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Said Sadiki (wa tatu kushoto), alipowasili Uwanjani hapo kwa ajili ya
kumpokea mgeni wake, Rais wa Marekani, Barrack Obama.
Ndege ya Rais wa Marekani, Barrack Obama, 'Airforce One' ikiwa imetua tayari, uwajani hapo.
Rais Barraka Obama akishuka na mtoto wake mkubwa Mallya, uwanjani
hapo, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza ziara yake ya siku mbili
nchini.
Mke wa Rais wa Marekani, Barrack Obama, Michelle Obama, akishuka kwenye ndege hiyo na mtoto wake, Sasha.
Mke wa Rais wa Marekani, Barrack Obama 'First lady' akikumbatiana na
Rais Jakaya Kikwete, mara baada ya kuwasili uwanjani hapo na mumewe
(kulia), leo mchana.
Rais Obama akipokea maua kutoka kwa mtoto Zakia Minja, uwanjani hapo.
Rais Barrack Obama akiongozana na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili uwanjani hapo jana mchana.
Rais Obama akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili na kupigiwa mizinga 21.
Rais Obama akitoka kukagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake mara
baada ya kuwasili na kupigiwa mizinga 21, uwanjani hapo jana.
Rais Barrack Obama akiwa na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete
akipokea gwaride la heshima uwanjani hapo, mara baada ya kuwasili jana
mchana.
Rais Barrack Obama akisalimiana na mke wa Rais Kikwete, Mama Salama mara baada ya kupokea gwaride la heshima uwanjani hapo.
Rais Barrack Obama, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd.
Hapa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Akisalimiana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi.
Hapa Rais Obama na mwenyeji wake, Rais Kikwete, wakifurahia ngoma ya Mganda ya asili ya Wangoni, mkoani Songea.
Hapa Rais Barrack Obama akiongozana na mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuondoka Uwanja wa ndege.
Wananchi wakiwa wamekusanyika nje ya jengo la Ikulu kwa ajili ya kumkaribisha Rais Barrack Obama.
Wananchi waliokusanyika nje ya jengo la Ikulu jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kumkaribisha Rais Barrack Obama,wakipunga bendera za
Tanzania na Marekani.
Maofisa na baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, wakiwa nje ya Ikulu, kumkaribisha Rais,
Barrack Obama.
Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma (kulia), akiwa na mgeni wake, First lady, Michelle Obama, kwenye Ofisi za Wama.
Hapa wakiwa Makumbusho ya Taifa, wakipokea mau kwa ajili ya kuweka
kwenye mabaki ya vifaa vilivyolipuliwa na bomu kwenye Ubalozi wa
Marekani jijini Dar es Salaam.
Wake hao wa Marais wa Marekani na Tanzania, wakiweka mashada hayo
kwenye mabaki hayo kwa ajili ya kuwakumbuka waliopoteza maisha yao
kwenye tukio hilo.
Wakiwaombea wahanga hao, mara baada ya kuweka mashada hayo ya maua
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog