Facebook Comments Box

Tuesday, July 23, 2013

SOMA WASIFU WA KOCHA MPYA WA BARCELONA

FC Barcelona imefikia makubaliano rasmi kumsaini Gerardo Martino kuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili, kwa mujibu wa mtandao rasmi wa FC Barcelona.
  
Kilichobakia kwenye makubaliano hayo ni kusaini mkataba baada pande zote mbili kukubalina kila kitu.

Ratiba rasmi ya kuwasili kwake Nou Camp, utiaji saini wa mkataba na kutambulishwa rasmi itatangazwa msaa kadha yajayo. 

Gerardo ambaye anajulikana kama ‘Tata’, alizaliwa jijini Rosario (Argentina) November 20, 1962. Ana uzoefu mkubwa wa soka la America ya Kusini, kwanza kama mchezaji na baada kama kocha, kazi yake ya mwisho ilikuwa kuiongoza klabu ya Newell's Old Boys, ambao alishinda nao ubingwa wa mwaka huu.

Gerardo Martino anakuwa kocha wa nne raia wa Argentina kuifundisha FC Barcelona baada ya Roque Olsen, Helenio Herrera na César Luis Menotti.

WASIFU WA KOCHA GERARDO MARTINO TATA

 
SOURSE:SHAFFIH DAUDA


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU