Inaripotiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Polisi katika wilaya ya Mufindi, PCD
Ambwene Manyasi amewataka waganga wa jadi kuacha mara moja kuwapatia
majambazi dawa za kutokukamatwa na polisi, na badala yake waganga hao
wawapatie askari polisi dawa za kuwaona na kuwakamata wahalifu.
Eliasa Ally wa gazeti la Majira anaripoti kutoka Mufindi kuwa kauli na wito huo umetolewa na OCD huyo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mufindi, wakati akizungumza na waganga wa jadi na tiba asilia kutoka Mudindi.
OCD amesema ni jukumu la kila mwananchi kuuchukia uhalifu na kulisaidia jeshi la polisi kutimiza wajibu wake. Amenukuliwa akisema ifuatavyo:
"Ninyi waganga wa jadi na tiba asili kazi yenu kubwa ni kutubu magonjwa yanayowasibu watu na siyo kutibu mbinu za majambazi ili wasiwe wanakamatwa wanapofanya uhalifu, hapo tutakuwa hatusaidiani, badala ya waganja kuwa wachonganishi, wawe waunganishaji wa wananchi, polisi na jamii. Badala ya kutoa dawa ya sisi polisi tusiwaone wala tusiwamamate majambazi, sasa nyinyi waganja mtoe dawa ya kutuwezesha kuwaona na kuwakamata kiurahisi majambazi wanaofanya uhalifu katika jamii yetu, huo ndiyo ushirikiano na polisi jamii tunayoizungumzia."
Aliwataka waganga hao kuhakikisha kuwa shughuli zao haziwi chanzo cha kutokea kwa maovu, kufumbia macho maovu na kusababisha jamii iwachukie waganga na polisi.
OCD alisema Jeshi la Polisi limejikita katika mambo makubwa matatu ambayo aliyataja kuwa ni polisi jamii, hali ya weledi na hali ya usasa.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog