Facebook Comments Box

Sunday, July 28, 2013

NAPE NNAUYE AKERWA NA KUSIKITISHWA NA HABARI YA GAZETI LA MTANZANIA

Nimestushwasana na stori ya gazeti la Mtanzania inayodai kuninukuu kuwa nimesema wazee waliopendekeza serikali tatu wanasubiri kufa!

Kwa kweli nimesikitishwa sana hata na jinsi maneno ndani yalivyopangiliwa kiasi kwamba inanipa tabu kuamini kama mhariri aliipitia hii stori ukiachilia mbali kama aliyetumwa kuja kuandika stori alikua ni "too junior".

Nawaheshimu sana wazee wangu hawa hata kama nikipishana nao kimawazo siwezi kufikia kutamka maneno makali kiasi hicho.

Nilichosema ni kuwa ukilinganisha vijana na wazee, vijana wanawajibu mkubwa wa kuamua kesho yao badala ya kudhani kuna mtu atawaamulia. Hivyo wanawajibu mkubwa kwani takwimu zinaonyesha asilimia 60% ya idadi ya watu nchini ni vijana! Sasa sijui kama kwa mwandishi na mhariri wake tafsiri ndio hiyo?!!!

Imenisikitisha sana!

Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU