Badhi
ya viongozi wa TFF wakisaini mikataba na Meneja Mkuu wa Kampuni ya
Azam, Said Mohammed (wa kwanza kulia) leo kwenye Ofisi za TFF zilizopo
Karume jijini Dar es Salaam.
Televisheni
ya Azam inayojulikana kama Azam TV imeingia mkataba wa miaka mitatu wa
kuonesha michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) ambapo mkataba huo umetajwa kuwa na thamani ya Tsh
bilioni 6.5
Aidha
Televisheni hiyo itakuwa na majukumu ya kuonesha mechi za moja kwa moja
(LIVE) zisizopungua 60 za Ligi hiyo huku nyingine 180 zikiwa
zimerekodiwa.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog