Langa
Kileo (msanii wa Hip Hop Tanzania, pichani) amefariki dunia leo hii. Langa
alipelekwa hospitali akiwa hajitambui. Anadaiwa kuwa alikumbwa na Malaria kali
sana, Hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana. Uchunguzi wa
chanzo cha kifo chake bado unaendelea. Msanii Langa aliwahi kutamba na kikundi
cha Wakilisha pamoja na witness na sara ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa
bongo flava nchini Tanzania. Mungu amrehemu.
Baba
wa marehemu Mzee Kileo amesema kuwa mtoto wake Langa kwenye picha amefariki
dunia leo majira ya saa 10 katika hospitali ya Taifa Muhimbili.Taarifa kamili
na mipango ya mazishi zitatolewa pale vikao vya familia vitakapofanywa.Pia baba
yake alisema msiba huu umetokea wakati mama yake Langa hayupo Tanzania,alisema
kwa sasa mama yake Langa yupo Marekani lakini baada ya kupewa taarifa hizo
tayari ameshakata tiketi ya kurudi Tanzania na ataanza safari kesho.Msiba uko
nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni
Aminiel
Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili amethibitisha
kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi na moja jioni baada
ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo kutokana na sababu za
kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali hawawezi kusema rapper huyu alikua
anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Kwenye
maelezo aliyoyatoa kwa millardayo.com Aminiel amesema Marehemu Langa
alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa kuamkia
jana na kupatiwa huduma ambapo leo June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba
cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog