Charles Mullinda |
Mhariri Mtanzania Jumatano
Kaimu Mwenyekiti
Jukwaa la Wahariri
YAH: KUJITOA KWENYE
JUKWAA
Napenda kukufahamisha kuwa nimeamua kujitoa kwenye Jukwaa
la Wahariri kwa sababu siridhiki na mwenendo wa Jukwaa hilo.Nimeamua
kujitoa kwa sababu sijaridhishwa na uamuzi uliofikiwa wa kuingilia uhuru wa
habari na kufumbia macho baadhi ya mambo ambayo ninaamini
hayapaswi kufumbiwa macho.
Uamuzi wangu huu pia unatokana na jinsi jukwaa
linavyotumia nguvu kubwa kuficha ukweli unao wahusisha
baadhi ya wahariri ambao gazeti hili lilibaini kuwa
walikuwa na mawasiliano yenye utata na aliyekuwa mtuhumiwa wa ugaidi, Joseph
Ludovick. Aidha siridhishwi na jinsi baadhi ya wahariri wanavyoshambuliwa na
wahariri wenzao katika magazeti yao pasipo Jukwaa kuchukua hatua huku kwa
upande mwingine likitumia nguvu kubwa na pesa nyingi kuwalinda baadhi ya
wahariri ambao nyendo zao zinatia mashaka.
Kikao cha kwanza na TEF na kilichofanyika leo
kimedhihirisha pasipo mashaka kuwa TEF iliamua kuwa na ajenda maalumu ya
kumshughulikia Mullinda kwa kuwa tu nilionyesha mawasiliano ya Deodatus Balile
na Ansbert Ngurumo dhidi ya Ludovick kama ambavyo gazeti la Tanzania Daima
lilivyoonyesha mawasiliano ya Dennis Msaki na Ludovick.
Ripoti ya timu iliyoundwa kuchunguza ukweli wa habari
iliyoandikwa na gazeti la Mtanzania Jumatano ina upungufu mkubwa wa kimantiki
ambao hata kwenye kikao niliuonyesha lakini haukusikilizwa.Ushahidi wa Ngurumo
kumtumia pesa Ludovick upo wazi, lakini hakuna mtu anayeliangalia hilo kwa
sababu tu timu ile iliundwa kumshughulikia Mullinda kwa sababu aliandika vigogo
wa TEF ambao wako karibu na viongozi wa TEF.
Nimeamua kujitoa baada ya kubaini kuwa jukwaa linafanya
kazi kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi.
Kwa taarifa hii naamini utaratibu wa kawaida wa kuagana
utazingatiwa.
Charles Mullinda.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog