Facebook Comments Box

Sunday, May 19, 2013

MSIMU WA 2014/2015 NDIO KILA MSHABIKI WA ARSENAL ATAKUWA NA FURAHA

Ilikuwa mwaka 1996 Manchester United wanashinda taji lao la kumi (10) la ligi kuu ya Uingereza kwa kuipita Everton iliyokuwa na mataji tisa (9) na kuwa sawa na Arsenal katika mataji. Mpaka mwaka 1997 Arsenal walikuwa hawajashinda Taji lolote la ligi kwa miaka 6 na Bodi ya klabu ya Arsenal hatimaye ikaamua kuwa ni muda muafaka wa kuhamia kwenye uwanja mkubwa ili kuweza kwenda sawa na malengo ya vilabu vikubwa barani ulaya. Mpaka mwanzoni wa miaka ya 90 Everton mataji (9) na Arsenal mataji kumi (10) zilikuwa ni timu zenye hadhi sawa katika soka la Uingereza chini ya Liverpool iliyokuwa na mataji (18) na juu ya timu iliyokuwa inachipukia ya Manchester united iliyokuwa namataji (7). Arsenal FC ilikuwa kilabu cha kumi na sita kwa utajiri barani ulaya katika kipindi hicho na Nguvu za kujitolea zilihitajika ili kuisukuma Arsenal katika nyakati za kisasa. Na mtu aliyechaguliwa kuifikisha hapo ni kocha asiyekuwa na sifa wala jina katika ulaya ambae ni Mfaransa Arsene Wenger. Kutoka kushinda taji la ligi kuu la Uingereza katika mwaka wake wa pili kama kocha wa Arsenal mpaka msimu ambao alichukua ubingwa bila kufungwa mechi hata moja akiwa ameshinda michezo 26 na kutoka sare michezo 12 (invisible) kiukweli ni kipindi ambacho kinafahamika kama kipindi cha ukweli na ubora wa uongozi wa Arsene katika klabu ya Arsenal. 
Baada ya miaka saba(7) ya mpango wa kuwa na uwanja mpya na mkubwa ukiwa na hadhi ya kisasa zaidi hatua za kiutaalamu katika eneo linalo itwa Ashburton Grove ulikamilika. Gharama za awali za ujenzi za uwanja zilikadiliwa kufika Paundi za uingereza milioni 420 ,Mambo ya kifedha yalikuwa ni magumu kwa kuwa klabu ilkuwa haifadhiliwi na mtu au kampuni kutoka nje mapato yalitokana na timu yenyewe. Lakini Arsenal FC iliamini kwa kiasi kikubwa katika sera yake ya kibiashara ya kujiendesha yenyewe (self-sustainability). Ili kuweza kuuufanikisha huu mradi mkubwa wa ujenzi wa uwanja, Arsenal FC ikachukua hatua mbalimbali kwa umakini mkubwa kama kuweka ukomo wa mishahara kwa wachezaji. Lakini ujio wa Roman Abromovic kuimiliki Chelsea, Kiuhalisia uliharibu mipango ya Arsenal kujiendesha yenyewe.

Mwaka 2006 umbali wa maili 800 kutoka jiji London uwanja mpya ambao ulipewa jina la Ashburton grooves kwa jina maarufu unaitwa Emirates stadium kwa sababu shirika la ndege la fly emirates lilinua haki za matangazo ya uwanja kwa mkataba wa miaka 6 ukafunguliwa na uwanja wa zamani Highbury stadium ukafungwa na kubadilishwa kuwa makazi ya watu maarufu kama highbury square. Maisha ya uwanja mpya wa Emirates yakaanza timu ilijua kuwa kipindi cha mpito kimeanza na kitaenda na miaka mingi sana pasipo kupata makombe na Arsene Wenger alifahamu kuwa Kufuzu kucheza michuano ya vilabu bingwa barani ulaya kila msimu kitakuwa ni kitu cha muhimu zaidi katika maisha mapya ya klabu ya Arsenal katika miaka saba inayofuata toka 2006. Kutoka miaka 7 iliyopita mpaka sasa washabiki wa Arsenal wameshuhudia kila kitu wachezaji kuumia vibaya mfano mkubwa ni kuvunjika kifundo cha mguu cha Abouu Diaby, kuvunjika miguu kwa Aron Ramsey na Eduardo da silva, Manahodha wa timu kuondoka mmoja baada ya mwingine. Wengi wanasema na kukandia kama ni timu inayolea na kuuza wachezaji wake wakubwa kwa wapinzani wake wakubwa au timu zenye utajiri mkubwa. Ni nyakati ngumu kuwa shabiki wa Arsenal wakati marefa na dunia nzima wako tofauti na wewe lakini ndio kipindi cha kufurahia imani na nia yako wakati wa mapambano kwa kila jambo gumu linalokukabiri. Nimesema kwamba Kufuzu kucheza michuano ya vilabu bingwa ulaya ni kitu cha muhimu na ndio lengo kubwa katika kuokoa kwenye kipindi hiki cha mpito . Kumbuka Chelsea baada ya kutumia pesa nyingi katika kufanya usajili (usajili wa kufuru) walikuwa wa sita kaitika ligi kuu msimu uliopita na kiukweli waliokolewa na tukio la kukosa penati la wajerumani jijini Munich. Kama Chelsea wangekosa kuchukua ubingwa katika fainali ile, wangekuwa wanacheza katika Europa ligi wakiwa hawana Eden Hazard na Oscar.Huo ndio umuhimu wa kufuzu klabu bingwa ulaya, hiyo michuano inakupa pesa pamoja na mvuto kwa wachezaji kutokana na hiyo michuano. Kama Roman na Sheikh Mansour wasingesababisha haya matatizo pengine arsenal ingekuwa ni mshindani katika mbio za ubingwa wa uingereza. Kuweka vitabu sawa vya kifedha ni jambo jema zaidi katika uhai wa klabu na Naishukuru Bodi ya utendaji ya Arsenal inatekeleza jukumu hilo kwa ufasaha zaidi. Roman Abrahomovich ndiye alie maliza vita kali iliyokuwepo kati ya Arsene Wenger na Ferguson ilioanza miaka nane(8) ilioanza toka 1996 mpaka 2004 .Ambapo Ferguson alipata makombe matano ya ligi kuu na Wenger kupata makombe 3 ya ligi kuu.
Na mzizi wote uliosababisha matatizo haya unatokana na “Kwa jinsi gani klabu ya mpira wa miguu inavotakiwa iendeshwe” na hiyo ndio picha halisi iliyopo. Zaidi ya timu 170 za mpira wa miguu Uingereza sasa zinahusisha mojakwamoja katika shughuli mbalimbali za timu kupitia vyama vya mashabiki. Lakini uhusika mashabiki katika klabu zao ni mdogo kulinganishwa na Bundesiga na ligi zingine barani ulaya. Mfumo wa Ujerumani ni bora zaidi kutokana kwamba vilabu vyao vyote viko safi kiuchumi. Katika La-Liga mfumo wake ni wa kinyonyaji na uliojaa rushwa kwakuwa timu mbili tu za juu ndizo zinazopata mapato makubwa kuliko timu zote. Timu zilizo katika mstari salama ndizo zinazoendeshwa na vikundi au vyama vya wanachama na haki za Television zinajadiliwa kulingana umaarufu wa timu, pamoja na haki za kibiashara. Barcelona na Real Madrid zinapata euro milioni 300+ kila mwaka kutoka kwenye haki za Television na Biashara, lakini hali haiko hivo kwa timu inayoshikilia nafasi ya tatu Valencia inayopata euro milioni 75 tu kila mwaka. Kwa kiasi Fulani muda mwingine timu za chini katika La-Liga zinapingana na kugoma kwasababu ya timu mbili kubwa na kama ligi itakuwa sawa timu zote mbili zitapoteza euro milioni 150 kila mwaka na nguvu zao kuanza kushuka taratibu ndipo timu nyingine zitazikamata.
HUO NDIO UWANJA WA EMIRATES
Ni sawa vilabu vya mpira wa miguu vinaweza kuendeshwa kwa kutumia njia kuu tatu
i)Mfumo wa kibiashara wa kujiendesha wenyewe (self-sustaining ):Unanunua kwa kile upatacho
ii) Kutumia wawekezaji wanje (sugar dadies): Mwanzoni unafanikiwa mwishoni unashindwa
iii) Kubadilisha wamiliki (Changing ownership): Old method
Hakuna njia iliyosahihi na ndio inayokuhakikishia mafanikio bali yoyote inaweza kutoa matunda mazuri lakini Mfumo wa self-sustaining model unaifanya klabu iweze kudumu kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa ndani ya uwanja nanje ya uwanja. Kama mmiliki waklabu anaondoka anachokifanya ni kuuza hisa zake mwenyewe. Kutumia pesa nyingi kuendesha timu hakutoi uhakika wa mafanikio. Kuna mifano mingi Kama Leeds United ambayo inatuonya katika kutumia pesa kwa wingi kuendesha timu kinyume na uwezo wa timu ni jambo la hatari na ni onyo kali kwa wale wote wanaofikiria kwamba klabu kubwa ni kufanya manunuzi ya bei mbaya katika soko la usajiri. Malaga imethibitisha hilo wakati ambao wamiliki walipofilisika na tulimpata Santi Carzola kwa bei rahisi. PSG ni timu inayochekesha kwa Ufaransa ilianza vibaya msimu baada ya kufanya manunuzi makubwa. Manunuzi makubwa sio suluhisho la Timu kufanya vizuri . Blackburn, Portsmouth, Rangers, Cardif na QPR ni mifano ya timu zilizoshindwa licha ya kutumia pesa nyngi. Muulize mchumi wa daraja lolote atakuambia Arsenal inaenda katika njia iliyonyooka kuweza kupata mafanikio iliyojiwekea (SOLVENT CLUB) 
Wacheza kamari wengi na mashabiki wa timu pinzani hawata penda kulisikia Jambo la kwamba Arsenal ni timu inayoendeshwa vizuri na wataizungumzia Arsenal kama Timu inayowanenepesha wengine au klabu inayouza tu. Kwa utashi sahihi Arsenal ni timu inayouuza inayomiliki maji. Tunauza wachezaji wa timu ya kwanza na wanazalisha faida kubwa ambayo inatumika kulipia madeni . Lakini kila mtu anafikiri kwamba wanataka kuuza wachezaji  kubwa? Samir Nasri alitaka Mshahara mkubwa ambao isingewezekana kuulipa kulingana na viwango vya mshahara vya Arsenal, Cesc alitaka kurudi Nyumbani na hata Mshambuliaji RVP alitaka mshahara mkubwa ambao upo juu zaidi ya ukomo wa klabu na alikuwa akijaribu kulazimisha kwa jinsi gani kocha aiendeshe timu na wachezaji ambao walitakiwa kusajiliwa na timu. Song alijenga nyufa mazoezini hatimaye akaondolewa klabuni.
Ingawa watu wegi wanailaumu Arsenal kwa kuwa na tiketi za gharama kubwa zaidi, ila mashabiki wa timu wanajua kwamba 41% ya mapato ya kuendeshea klabu ya Arsenal yanatokana na mapato ya viingilio vya uwanjani. Kwa kifupi mshabiki kulipa kwa kiwango kikubwa kwa ajili ya kuitosheleza timu katika kipindi hiki cha mpito ni jambo jema na la busara. Emirates ni moja kati ya viwanja bora Uingereza, na Sifa zote ziiendee bodi ya Arsenal kwa kuijenga timu pasipo kutegemea pesa za mafuta au gesi toka Urusi na Uarabuni. Graham Hunter alitoa maelezo kwamba Arsenal sio timu inayouza wachezaji lakini ni klabu ya kibiashara(Trading club).  Usiwe unafikiri au kuamini kila ambacho vyombo vya habari huandika kwasababu vyombo vya habari siku zote haviipendi na ni wapinzani wa Arsenal. 
Na hili ndio kombe la Dhahabu la Arsenal walilopewa baada ya kutofungwa msimu mzima


Pale ambapo Arsene husema katika Mpira wa miguu tumesheherekea ushindi sana . Ina maanisha Arsenal imekosa malengo au nia mathubuti? ingekuwa tofauti kama wangeshinda Ubingwa wa ulaya pale Paris? Au Kama wangechukua Carling cup miaka miwili iliyopita? Hayo matukio yote mawili ya dakika 10 yangeifanya ionekane ni klabu yenye nia? Maswali mengi yanakuja Nini ambacho Arsenal inataka ikipate? Kufuzu klabu bingwa ulaya kila mwaka au mataji? Suala linafuata ukubwa, nafasi na mapato kwa timu yetu , ni kitu gani kinatakiwa kutiliwa mkazo? Katika viwango vya mishahara ya wachezaji tuko nafasi ya 5 kwa uingereza na nafasi ya 10 ulaya. Msimu uliopita timu iliishia nafasi ya Tatu (3) Kwa mafanikio hayo tulizidi uwezo wetu. Timu kama Swansea, West Brom alibion (WBA) na Wigan upande wa Uingereza na Borusia na Dortmund kwa ulaya kwa kutumia rasilimali finyu walizonazo wamepata mafanikio makubwa mwaka huu , Newcastle united ilifanya vizuri juu ya uwezo wao msimu uliopita na Middlesborough walifanya hivvo hivvo mwaka 2005 na 2006. Ukweli ni kwamba kila mwaka kutakuwa na klabu zinazofanya vizuri sana na zingine zinazo fanya vibaya. Kipimo cha ukweli ni majaribio ya kudumu kwenye kiwango kwa muda mrefu ambao kila timu inaweza kuufanya na kudumu huko Arsenal inafanya na imekuwa ikudumu kwenye kiwango chake kwa miaka 16 (Kiwango bora kabisa toka imeanzishwa)
Kutokuwepo kwa nia ya ushindi sio maneno sahihi kwa upande wa arsenal. Klabu ya Arsenal inapungukiwa Rasilimali nani ukweli kuhusu hilo. Je ni kweli kuwa CR7 (Ronaldo) hana malengo na madhumuni kwasababu kila mwaka ana kuwa wa pili baada ya Messi katika tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa dunia katika kura? Arsenal ina furaha kwa kushika nafasi ya nne kwasababu timu tatu inazoshindana nazo zina malipo kwa wachezaji 50% mpaka 200% kuizidi. Kiuhalisia ni kwamba kama itazizidi inakuwa ni jambo la hasara na itazishusha hadhi ( kama ambavyo ilivyokuwa juu zaidi ya Chelsea msimu uliopita ) Toka mwaka 2006 kuna makombe 24 ambayo wangeweza kushinda. wamepoteza fainali tatu(3) na wamepoteza ligi kuu mwaka 2007/2008 kwa bahati mbaya. Wengi watasema sawa wangeweza kushinda kombe la ligi au Kombe FA? Lakini kuna mtu yeyote anayeweza kusema walijaribu lakini hawakushinda? sababu katika mpira kushinda na kushindwa ndio kanuni. Wamepoteza Fainali mbili za kombe la Carling katika miaka ya karibuni kutokana na kutumia wachezaji wadogo sababu kubwa ni ufinyu wa bajeti. Swali linakuja je Arsenal ingenyanyuka kiuchumi au kurudi kama zamani kama ingeshinda Carling cup au ndo ingeonekana ina mipango thabiti?. Katika miaka ya karibuni kombe la FA na Carling limekuwa na wanafainali kama Portsmouth, Birmingham, Totenham ,Swansea , Bradford,Cardif city na sasa Wigan. Liverpool imeshinda kombe la carling msimu uliopita wakiifunga Cardif city kwa penati na Wigani ikiifunga Machester city katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA na kusababisha kocha wa Mancin kufukuzwa kazi, kila mtu anakubali kuwa michezo ya makombe ni michezo ambayo haitabiriki. Sasa Je, Liverpool ni timu yenye malengo makubwa kwa kushinda kombe la Carling kuliko Arsenal? Muulize shabiki yeyote wa Liverpool kama anataka timu yake ishinde FA au Carling(kama wanayataka haya mashindano) au wanataka Kufuzu nne bora ili washiriki michuano ya klabu bingwa barani ulaya. Nina uhakika kwamba 90% watataka kufuzu nne bora. Kucheza Katika mashindano ya klabu bingwa ulaya ni kitu ambacho kila timu inakitaka na kukihitaji na kama ukikikosa unakuwa kama umepoteza maisha. Kuinuka kwa Mancity na Chelsea kumetengeneza vikwazo vikubwa sana kwa Arsenal na kama kesho Tajiri mwingine akainunua Westham nina imani ushindani utakuwa umeongezeka sana lakini kama QPR , kila klabu haiwezi kutumia mamilioni ya pesa na kufanikiwa. Timu nyingi zitaishia kama Leeds, Portsmouth, Rangers au Malaga. 
Hii ni nembo ya kampuni ya Puma iliyoingia mkataba na Arsenal. Ni mkataba ghali zaidi kuliko yote uingereza katika udhamini wa jezi. Arsenal watavaa msimu wa 2014/2015

Machester united walianza kujikita katika soko la biashara la dunia miaka kumi nyuma. Walipata mapato makubwa kuliko sisi na kuwa juu yetu kipindi ambacho tumejikita zaidi na mpango wa kujenga uwanja wetu. Hata Liverpool pia wanajaribu kuongeza ukubwa wa uwanja wa Anfield ili uweze kuingiza watu 60000 na zaidi kabla yamwaka 2017 na sio hao tu pia Chelsea wanajaribu kufanya hilo pia. Lakini Arsenal wameshaweza kushinda mzigo mkubwa wa madeni uliotokana na uwanja , Sasa timu inarudi kama zamani na itasimama sawa kama Wapinzani wao Manchester united. Mpaka sasa wanatakiwa kufuzu kucheza mashindano ya klabu bingwa ulaya ambayo ni uti wa mgogongo wao. Kwa mwaka 2014 mikataba mingi ya ufadhili (jezi na kibiashara) mingi itakuwa imerekebishwa upya na kuwafanya wawe na uwezo mzuri kimapato, Madeni yatakuwa katika kiwango cha chini mno na watakuwa na uwezo wa kujitangaza katika safari mbalimbali za kiutalii za timu. Kutokana na kuongezeka kwa mapato ya timu wataweza kuongeza ukomo wa mishahara kwa wachezaji. 2014 utakuwa mwaka ambao kila shabiki wa arsenal anaousubiria kwa hamu sababu utakuwa na mapato ya kuendeshea timu(madeni madogo pamoja na mikataba mipya ya kibiashara) yatazidi zaidi ya paundi za uingereza 300 milioni kwa mwaka ambao utawafanya na wao waingie kwenye kundi la timu Tajiri ulaya ambazo kwasasa ni Barcelona, Bayern munich, Real Madrid na Manchester United. Kwa mikataba mipya na kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Puma na kampuni la ndege ya Fly Emirates Arsenal itapata pesa ya ziada inayofikia Paundi 50 milioni kutoka msimu wa 2014/2015.
Matokeo ya msimu huu yalimshusha moyo kila mtu ambaye ni shabiki wa klabu ya Arsenal. Baada ya kuanza vizuri katika viwanja vya Anfield, Britania na Etihad wakapoa njia baada ya kuumia kwa wachezaji Abou diaby na Kieran Gibbs pasipo kumsahau beki wao kisiki Koscienly pia kutojiamini kwa nahodha wa timu Vamaelen lakini nashukuru kwasasa baada ya kufungwa kwa mara ya mwisho na Totenham na hawajafungwa tena. Pia nashukuru ushindi wa munich uliifanya timu ijiamini na wako nafasi kubwa ya kujihakikishia kucheza michuano ya klabu bingwa ulaya msimu ujao baada ya mbio nzuri sana za kumalizia msimu. Wengi wanataka Arsenal Yao ya zamani irudi. Ipi ambayo ilishinda Makombe kumi ya ligi kutoka mwaka 1886 mpaka 1996. Wastani wa kombe moja la ligi baada ya miaka 11 hapo naona wanachemka na hawitakii mema kilabu yetu ya Arsenal. 
Nina swali moja linalo nisumbua mno. Nini kafara ya mafanikio? Toa kafara maisha yako ya sasa kwa maisha mazuri ya baadae na usitoe kafara maisha yako ya baadae kwa maisha mazuri ya sasa . Siku zetu za mafanikio zinakaribia pale ambapo mikataba yetu ya jezi na matangazo itakaporekebishwa lakini inaniuma mimi kama shabiki wa Arsenal pale ambapo Mashabiki wa Arsenal wanapotaka Arsene wenger Afukuzwe baada ya kila kitu tunachokijua katufanyia . Kwa upande wangu mimi naona Arsene Wenger kafanya kazi kubwa mnoo Arsenal kuliko uwezo wake pale ambapo timu inaendeshwa kwa bajeti ndogo sana 70% ya timu za Manchester na Chelsea. Kiwango cha matumizi katika Arsenal ni 40 milioni paundi, moja kati ya gharama ndogo sana katika ligi tano bora barani ulaya nabado inafuzu kucheza michuano mikubwa ya ulaya kila mwaka ingawa inacheza katika ligi iliyojaa Matajiri wakubwa na Pesa. Nina imani kama tutampoteza Arsene msimu ujao tutapotea na Mafanikio yetu makubwa yatakuwa yameenda na maji, tutabaki na kilio cha samaki ambacho machozi huenda na maji, Itabaki kuwa ni siku za kukumbukwa.Mnataka tumwache mpiganaji wetu na tumfukuze katikati ya mapambano kitu ambacho kitaivunja na kuiondoa klabu yetu ya Arsenal katika ramani ya soka dunianina kuwa timu ya katikati kama Liverpool, Everton na Swansea pengine kushuka hata daraja kwasababu timu tuliyokuwa nayo msimu huu asingekuwepo mzee Ingekuwa ya kumi.Ni uwendawazimu kamashabiki wa Arsenal una mawazo ya kwamba wenger aondolewe hivi ni kocha gani atakubali kuja kufanya kazi katika mazingira magumu kama Arsenal? Ivi hamshtuki tu timu kama Chelsea, Real Madrid, Barcelona, PSG na sasa timu yake ya zamani Monaco iliyonunuliwa na Tajiri wa kirusi zinamnyemelea kama ni kuondoka Arsene wenger angeondoka toka 2007 pale ambapo Real Madrid walikuja na ofa ya mshahara mara mbili ya anaolipwa Arsenal na Project nzuri na bado akakataa kwenda bado PSG nao wamekuja msimu huu lakini Bado mzee amejitoa kuitumikia Arsenal .Waswahili wanasema Mpende Akupendae asie kupenda Achana nae naomba tumpende wenger kwa kazi nzuri aliyotufanyia sio watafuta CV kama Akina Jose Mourihno. 
Mwisho Arsenal ni Klabu sahihi katika ulimwengu uliopotoka au katika maana nyingine katika ligi iliyopotea au kufa.
 
COME ON YOU GUNERS (COYG).


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU