Jeshi la Polisi Mkoa wa Dar es Salaam limetoa taarifa baada ya kuwepo
uvumi kuwa Kanisa la KKKT usharika wa Kunduchi Beach, lililopo Kunduchi,
Dar es Salaam limelishambuliwa kwa kupuliwa kwa bomu na kurushiana
risasi.
Kamanda wa Polisi Suleiman Kova amesema ukweli ni kuwa hakuna ulipuaji bomu uliofanyika katika Kanisa la KKKT Kunduchi Beach ISIPOKUWA kikosi cha Polisi kilichokuwa kinapambana na wahalifu waliokuwa karibu na Kanisa hilo kililazimika kurusha bomu la machozi ili kupambana na kuwatia mbaroni wahalifu hao.
Kova ameongeza kwa kusema waumini waliokuwepo Kanisani walishituka kwa kudhani kuwa wamevamiwa, lakini baadaye walipofahamu kinachoendelea walijitokea ili kusaidia, "Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha. Siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema Kova.
---
Taarifa hii imekukuliwa kutoka ITV na Radio One Stereo.
Tusubiri taarifa iliyoahidiwa kutolewa ili kuondoa tashwishi.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog