Mcheza filamu mashuhuri sana duniani,Angelina Jolie 
amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa
 uzazi.
Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New 
York Times, Bi Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa seli zake na 
kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani 
ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.
Angelina mwenye umri wa miaka 37 na mama wa watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.
Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.
Kulingana na Jolie madaktari walisema kuwa 
uwezekano wake kupata Saratani ya matiti ni asilimia 87 huku akiwa na 
asilimia 50 uwezo wake wa kuugua Sarati ya mfuko wa uzazi.
''Niliamua kuchukua hatua mwenyewe ili kuzuia uwezekano wowote wa kuugua Saratani hiyo,'' alisema Jolie.
Alisema kuwa shughuli hii ilianza mwezi Februari na kukamilika mwishoni mwa mwezi April.
Uwezekano wapunguzwa.
Katika taarifa iliyoandikwa na Bi Jolie na yenye
 kichwa, 'Uamuzi wangu wa kimatibabu', Bi Jolie alieleza kuwa mamake 
alipambana na Saratani kwa miaka kumi na kufariki akiwa na umri wa miaka
 56.
Alisema kuwa alielewa fika kuwa siku moja 
atawahi kuugua Saratani na ndio maana akachukua uamuzi wa kufanyiwa 
upasuaji huo mgumu wa wiki tisa ambao ulihitaji kukatwa matiti.
Uwezekano wake wa kuugua saratani sasa umeshuka kutoka 87% hadi 5%.
Alimsifu mumewe Brad Pitt, kwa kumuunga mkono na
 kumfariji kwa kila aliyopitia, na kusema kuwa ametulizwa na kuwa wanawe
 hawakupata lolote katika matokeo ya uchunguzi wa madaktari tangu 
kufanyiwa upasuaji.
"ninahisi kuwa na nguvu kwa uamuzi niliofanya, 
na kwa kuwa ninasalia kuwa mwanamke hata baada ya kuondoa viungo 
hivyo,'' alisema Bi Jolie.
"kwa mwanamke yeyote anayesoma maneno haya, natumai ataweza kujua kuwa wanaweza kufanya uamuzi.''
Muigizaji huyo, ambaye ameshinda tuzo nyingi kwa
 uigizaji wake, pia ni mtunzi wa filamu na mjumbe maalum wa Umoja wa 
Mataifa anayehusika na harakati za kibinadamu.
Wakati alipokuwa anafanyiwa upasuaji, Bi Jolie 
alizuru Jamuhuri ya Kidremokrasia ya Congo pamoja na waziri wa mambo ya 
nje wa Uingereza William Hague.
Jolie pia alihudhuria mkutano wa mawaziri wa 
mambo ya nchi za kigeni wa G8, kuhamasisha dunia kuhusu dhulma za 
kingono katika maeneo ya vita.
SOURSE: BBC SWAHILI 
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog