Facebook Comments Box

Tuesday, April 16, 2013

USIWEKE NDIZI KWENYE JOKOFU (FRIJI)

Na Hassan Bilal Ka'bange
Watu wengi watashangaa kwa nini wasiweke ndizi kwenye jokofu zao. lakini baada ya kusoma makala hii watajua kwanini haitakiwi kuweka ndizi kwenye jokufu na wataziangalia ndizi zao tofauti na walivyokuwa wakiziangalia zamani.
Ndizi zina sukari halisi ya aina tatu sucrose (Sukrosi), Fructose (Fruktosi) na Glucose (Gluktosi) ambazo zimeungana na fiber. Kwa hali hii ndizi zinakupa nguvu halisi na nzuri kwa ajili ya mwili wako.
Tafiti zinaonesha ndizi mbili zinatosha kukupa nguvu za kutosha kufanya kazi ngumu kwa muda wa dakika 90. Kwa hili siwezi kushangaa kuona ndizi kuwa ndio tunda linaloongoza kuliwa na wanamichezo wakubwa duniani.
lakini nguvu sio kitu pekee tunachokipata katika ndizi ambacho kinatupa umakini. Ndizi bado inatupa nguvu ya upambanaji na kinga dhidi ya magonjwa mengi sana. Na hilo ndilo linalofanya leo hii ndizi niisisitize iwe katika mlo kamili wa kila mwanadamu. Yafuatayo ni baadhi ya magonjwa ambayo ndizi inaweza kukukinga na kukutibu kwayo.

KUONDOA MSONGO WA MAWAZO:
kulingana na  tafiti fupi iliyofanya kwa wagonjwa wengi walio katika msongo wa mawazo yaani kitaalam DEPRESSION wengi wao wameonesha kupata nafuu na ahuweni baada ya kula ndizi. Hii inatokana na ndizi kuwa na kemikali ijulikanayo kama Tryptophan ambayo ni asili ya ptotini ambayo mwili huweza kuibadilisha na kuwa homoni ya Serotonin (serotonini) ambayo humfanya mgonjwa kutulia, kupata ahueni ya muhemko na kumfanya apate furaha.
Vilevile ndizi ina vitamini B6 ambayo husahihisha sukari ndani ya damu ambayo huleta athari katika mhemko.

KUONGEZA WINGI WA DAMU:
Ndizi ina madini chuma mengi, kwa muono huo ndizi huleta uchochezi katika utengenezwaji wa chembechembe za damu ambazo hujulikana kwa jina la Hemoglobin (himoglobini) hivyo husaidia ongezeko la damu mwilini.

KUONDOA SHINIKIZO LA DAMU:
Ndizi ni tunda la ajabu sana(unique) linalopatikana katika ukanda wa ki tropika ambalo lina madini ya potasiamu (Potassium) mengi na bado likiwa na chumvi kidogo, Hivyo inalifanya kuwa madhubuti katika kupambana na shinikizo la damu sana. Mamlaka ya Chakula na dawa ya Ameriaka ( US Food and Drug Authority) wameruhusu viwanda vya ndizi kuweka nembo zinazo onesha kuwa chakula hicho kinaweza kupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu na kiharusi.


KUONGEZA UWEZO WA AKILI WA KUFIKIRI NA KUKARIRI:
Wanafunzi 200 wa shule ya upili ya  Twickenham ya uingereza walisaidiwa ufaulu kwenye mitiani yao kwa kula ndizi wakati wa kifungua kinywa na wakati wa mapumziko na wakati wa chakula cha mchana kwa ajili ya kuongeza nguvu zao za kufikiri. Hii inaweza isieleweke vizuri lakini tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa madini ya potasiam (Potassium) yaliyopo kwenye ndizi yanasaidia uwezo wa kusoma kwa kufanya macho kuwa hai muda wote (Makes pupils more alert).

KUONDOA MAUMIVU YA TUMBO:
Watu wengi wamekuwa wakilalamika maumivu ya tumbo na kupata haja ngumu. Ndizi ina fiber nyingi ambazo husaidia kuweka sawa mwenendo wa utumbo na husaidia matatizo ya haja ngumu.

KUONDOA MNING`INIO:
Moja ya njia rahisi na nyepesi wa kuondoa mning`inio ni kutengeneza mkorogo wa ndizi na maziwa (Banana milkshake) ambao itahitajika kuongeza na asali kidogo kwa ajili ya kuongeza utamu. Pamoja na ladha nzuri na utamu utakao upata mkorogo huu wa ndizi utakusaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini wakati maziwa yatasafisha na kukuongezea maji mwilini.

KUONDOA KILUNGULIA:
Ndizi ina vimelea vya asili ambavyo hupambana na kilungulia. Kwa hiyo kama una matatizo ya kilungulia acha kula majivu ambayo hata haujui miti iliyotumika kama ina sumu hau hapana chukua ndizi moja ikuondolee matatizo.

KUONDOA HOMA ZA ASUBUHI:
Kula ndizi katikati ya kila mlo hufanya ndizi kusahihisha kiwango cha sukari mwilini na kukuondolea homa za asubuhi.

KUKUKINGA DHIDI YA UVIMBE WA KUNG`ATWA NA MBU:
Kabla ya kwenda dukani na kununua madawa ambayo yana madhara makubwa katika mwili wako na mazingira hebu chukua ganda la ndizi ule upande wa ndani jikunie/paka eneo ulilong`atwa na mbu. Watu wengi wamepata matokeo mazuri ya upunguzwaji wa muwasho na uvimbe unaotokana na kung`atwa na mbu..

KUKUONDOLEA MATATIZO YA NEVA ZA FAHAMU (NERVES):
Ndizi ina vitamini B nyingi ambayo hukusaidia kufanya neva zako za fahamu kuwa sahihi na salama.

KUKUONDOLEA ATHARI ZA KUPATA VIDONDA VYA TUMBO:
Ndizi ikitumika kama chakula hukuondolea athari za kupata vidonda vya tumbo kwa ajili ya umbo lake laini na murua. Vilevile husaidia kurekebisha (Neutralize) wingi wa asidi (acidity) na kupunguza mkwanguo kwa kuweka kava katika utumbo.

KUREKEBISHA JOTO MWILINI:
Tamaduni nyingi zimekuwazikiona ndizi kama kitulizo cha mhemko na kimwili wa wamama wajawazito kwa mfano nchini Thailand wamama wajawazito hula ndizi ili kuhakikisha watoto wao wazaliwe na joto sahihi. Kwetu hasa Maeneo ya Mbeya, Kagera na Kilimanjaro wamama wajawazito hupewa mkorogo wa ndizi na nyama maarufu kama Mtori ili waweze kunyonyesha salama na kurudisha afya yao na kuwakinga na magonjwa.

Ndizi ni dawa halsi ya magonjwa mengi. Ukitaka kufananisha na Tufani (apple) ndizi ina ptorini mara nne zaidi ya tufani ina sukari mara mbili ya tufani, ina madini ya fosforasi (Phosphorus) mara tatu ya tufani, ina mara tano zaidi vitamini A na madini ya chuma na ina mara mbili zaidi ya madini mengine. Bado ikiwa ni tajiri wa madini ya potasiamu na mengine.
Ni wakati sasa wa watanzania wenzangu kulipenda tunda hili na kulila ipasavyo. Na kwasasa sipati shida sana kuona nyani anavyo furahi na kuruka ruka unapomtupia ndizi inawezekana anajua thamani yake katika mwili wake.

TULE NDIZI ITUJENGEE MIILI YETU NA KUTUKINGA NA KUTUTIBU  MAGONJWA




Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU