Facebook Comments Box

Monday, April 15, 2013

MAPATO YA MECHI KATI YA SIMBA VS AZAM NA MECHI KATI YA YANGA VS OLJORO




Katika mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Aprili 14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000 kutokana na watazamaji 11,458.

Viingilio katika mechi hiyo iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14.

WATAZAMAJI 11,021 WAZISHUHUDIA YANGA, OLJORO
Watazamaji 11,021 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Oljoro JKT iliyochezwa juzi (Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 63,170,000.

Viingilio katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,853,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,636,101.69.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,552,501.25, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,531,500.75, Kamati ya Ligi sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,762,250.29.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU