Waziri
wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wapili
kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
Salaam kuhusu tamko la Serikali juu ya mgogoro wa mpaka wa ziwa Nyasa.
SERIKALI ya
Tanzania imeomba Malawi iache kutapatapa kuhusu mgogoro wa mipaka wa
ziwa Nyasa kufuatia Rais wa nchi hiyo, Joyce Banda kutangaza katika
baadhi ya vyombo vya habari kuwa atapeleka suala hilo kwenye Mahakama
ya Kimataifa ya Haki(ICJ), badala yake isubiri uamuzi wa jopo la
usuluhishi lifanye kazi na litoe maamuzi.
Aidha
serikali imesema kuwa hata siku moja haijapelekewa taarifa wala
nyaraka za siri kutoka kwa Katibu wa jopo hilo, ambalo linahusisha
marais wastaafu wa zamani wa Afrika na wanasheria kama ilivyodaiwa na
Rais Banda katika vyombo hivyo , kuwa kuna Mtanzania anayeitwa Dk.
John Tesha ambaye wanaamini ametoa habari na kuiba nyaraka za siri.
Akilitolea
ufafanuzi jambo hili, Waziri Membe amesema kuwa Tanzania na jopo
hilo limestushwa juu ya madai hayo na hatua ya Rais Banda kupoteza
imani.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog