Mwanamke wa kwanza mwenye asili
ya kiafrika aitwae CECILE KYENGE KASHETU kutoka nchini CONGO DRC
amechaguliwa kuwa Waziri nchini Italy, alizaliwa Agust 28 1964 (48 yrs)
na baadae aliolewa na Mwitaliano ambapo mpaka sasa ni Mama wa watoto
wawili.
Alihamia nchini Italy mwaka
1983 na kuchukua uraia, alihitimu mafunzo yake ya Udaktari unaohusiana
na madawa katika chuo cha Universita Cattolica del Sacro Cuore kilichopo
Roma, baada ya kumaliza chuo makazi yake yalikuwa eneo moja liitwao
Castelfranco Emilia Jimbo la Modena mkoa wa Emilia- Romanga akiwa
anaendelea na kazi yake ya udaktari.
Mwaka 2004 alijiunga na mambo ya
siasa katika chama cha PD yani Partito Democratico na alipata nyadhifa
mbalimbali mwaka 2010 lakini february mwaka huu ndio alichaguliwa
kuwa Mbunge kupitia chama chake cha PD, mwezi huu wa April 2013 ndio
huyu mama amechaguliwa kuwa Waziri anaehusika na mambo ya kigeni kwenye
Serikali ya Enrico Letta.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog