Taarifa za sasa kutoka Arusha
ni kwamba Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema anaendelea kushikiliwa na
jeshi la polisi Arusha na kuhojiwa kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu za
Wanafunzi wa chuo cha Uhasibu dhidi ya Mkuu wa Mkoa Arusha juzi.
Taarifa za uhakika kutoka kwa
mke wa Mh. Lema sasa hivi ni kwamba Polisi wamekataa kutoa dhamana yake
na kusema mpaka jumatatu ndio itajulikana.
Namkariri Mke wa Lema akiongea
na millard ayo akisema “jana usiku saa sita kasoro watu
walikuja kugonga nyumbani kwetu tukamtuma kijana aende kutazama ni kina
nani, aliporudi akasema ni Polisi.. sisi hatukuamini na tulikataa kwa
sababu hatukujua kama ni Polisi kweli au ni watu wanataka kuitumia hiyo
nafasi kufanya uhalifu, mimi nimeshinda Polisi kutwa nikifatilia gari
mbona chochote hakikutokea?”
Picha ya liblary |
“Alipojitokeza Polisi walimchukua na mimi nikaondoka nao, tulipofika kituoni walimtaka Lema kutoa maelezo lakini alikataa na kusema mpaka mwanasheria wake aje hivyo akapelekwa rumande, asubuhi tulipoamka na kuanza kufatilia.. R.C.O alisema yuko kwenye kikao na haongei na yeyote isipokua Mwanasheria wa Lema, walipomaliza kikao saa nane maelezo yakaanza kutolewa huku Mwanasheria akiwepo na kazi ikamalizika jioni saa 11 ambapo Polisi wamekataa kutoa dhamana mpaka Jumatatu” – Mama Lema
“shitaka kubwa lililo mbele yake ni uchochezi na kauli ambayo anadaiwa Lema kuitoa mbele ya Wanachuo cha Uhasibu kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga, na hata leo kwenye maelezo Lema amewaambia watu wa Arusha mjini hivyohivyo, kwamba dhambi kubwa kuliko zote ni uoga” – Mama Lema
Kwa kumalizia, Mke wa Mbunge Lema amesema “gari letu lililokua linashikiliwa na Polisi tumerudishiwa baada ya kutakiwa kulipia elfu 50 ya wale waliolivuta, gari liko zima kabisa………… toka nimeolewa na Lema nimeshuhudia akienda polisi zaidi ya mara 20, mara yake ya kwanza kushuhudia anapelekwa polisi ni wakati wa kampeni za Ubunge”
SOURSE:Millard Ayo
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog