Mshambuliaji wa zamani wa Brazil Romario
ameanzisha upya vita vyake na na gwiji wa soka duniani Pele kwa kumuita
ni mtu mpumbavu.
Wachezaji hawa wawili wa zamani wa Selecao wamekuwa kwenye ugomvi kwa muda mrefu kufuatia Romario kupinga rekodi za mabao ya Pele mwaka 2007.
"Kuna watu wengi ambao hawajui nini wanataka na mwishowe wanabaki kushambulia kwa maneno wakati uliopita. Lakini mimi ni mkatoliki na naamini kwamba Mungu siku zote anamsamehe mtu mjinga, hivyo na mie namsamehe mtu wa aina hiyo," Pele alisema Ijumaa.
Na katika kumjibu Pele, Romario aliandika kwenye ukurasa wa Facebook: "Jana, Pele amejibu kuhusu kauli yangu maarufu, 'Kimya, Pele ni mshairi". Ni msemo maarufu unaotumika sana, na yeye mwenye amekuwa akiupa sababu ya kukua.
"Kitu cha kipumbavu kabisa alichosema ni kwamba yeye ni mkatoliki mkubwa. Sidhani yeye ni mkatoliki wa kiasi hicho, kama angekuwa mtu namna hiyo angemtambua mtoto wake wa kike na angeenda kwenye mazishi.
"Sasa hivi sio tu mshairi, pia ni mpumbavu." - Romario
Miaka miwili iliyopita, Romario alisema Pele anaongea upumbavu mno, baada ya Gwiji
huyo wa soka kusema kwamba Romario alikuwa anajaribu kutumia uchawi
dhidi ya shirikisho la soka la Brazil kufuatiwa kuachwa kwake kwenye
kikosi cha Brazil kilichoshiriki World Cup 1998.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog