Facebook Comments Box

Sunday, March 31, 2013

UHURU KENYATA AIBUKA KIDEDEA MAHAKAMANI BAADA YA MAHAKAMA KUTOA UAMUZI KUWA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA HAKI

MAHAKAMA:
Kenya imeamua leo kuwa Uhuru Kenyatta alichaguliwa katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki,  na kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na mgombea Raila Odinga aliyedai kwamba kura zilichakachuliwa.
Uamuzi huo umesafisha njia kwa Uhuru Kenyatta kuingia Ikulu. Anatarajiwa kuapishwa wiki ijayo Aprili  9, 2013 uwanja wa michezo wa Moi.

 Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe Raila Odinga amekubali uamuzi wa mahakama kuu, na kukubali yaishe (shingo upande?) kuashiria kwamba sasa mambo ni tambarare, na sio kama ilivyohofiwa awali kuwa kutatokea vurugu kama za uchaguzi wa mwaka 2007.

uamuzi wa mahakama hii kwamba walalamikiwa wa tatu na wa nne walichaguliwa kwa
haki”, alisema Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga, wakati wa kutoa uamuzi huu, akimaanisha Kenyatta na
mgombea mwenza na Naibu Rais William Ruto wameshinda kihalali.

Jaji Mkuu huyo alisema mahakama imetekeleza wajibu wake katika muda huo wa
kihistoria. “Sasa ni juu ya Wakenya, viongozi wao, taasisi za kijamii, sekta
binafsi na vyombo vya habari kutekeleza wajibu wao kuhakikisha umoja, amani,
utaifa na maendeleo ya taifa vinahifadhiwa”, aliongezea.

Rais mteule wa Kenya huyo alimshinda mpinzani wake kwa asilimia 50.07 dhidi ya
asilimia 43,28 za Odinga.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU