Bunge
limesema wabunge watakaokataa kuhojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na
Madaraka ya Bunge, watakamatwa na polisi na kufikisha kwenye kikao cha
kamati hiyo.
Juiz, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Wilbroad Slaa aliwakataza wabunge wake kuitika wito wa kuhojiwa na kamati hiyo hadi Spika atakapojibu baadhi ya madai ya chama hicho.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge, John Joel, alisema mbunge anayehitajika kuhojiwa na kamati hiyo hupelekewa barua ya kuitwa na endapo akikataa kufika atakamatwa na polisi.
“Mbona jambo hili lipo wazi kwa kila mbunge kwa kuwa sheria zinajieleza kuwa ukikataa wito utafuatwa na askari ambaye atakuleta kwa lazima katika kamati hii.Dk Slaa alikataa wabunge kuhojiwa baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuitaka Kamati ya Maadili kuchunguza vurugu zilizojitokeza wiki wakati wabunge walipokuwa wakijadili hoja binafsi ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), iliyohusu upatikanaji wa majisafi na uondoshaji wa majitaka Dar es Salaam.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog