Tunda aina la Stafeli.
TUNDA
la stafeli linatibu magonjwa kadhaa, ikiwamo saratani kwa ubora wa
karibu mara 10,000 ya matibabu ya kawaida yanayopatikana kwenye vituo
vya afya, utafiti umebaini.Utafiti
huo uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dawa cha Purdue nchini Marekani,
umeeleza kuwa mbali na kutibu saratani, tunda hilo pia ni tiba ya
matatizo ya msongo na mfadhaiko.
“Maajabu
ya stafeli ni kwamba lina uwezo wa kuangamiza chembehai zenye saratani
pasipo kusababisha madhara katika mwili kama zinavyofanya dawa nyingine
za ugonjwa huo au mionzi,” imesema sehemu ya utafiti huo uliochapishwa
kwa mara ya kwanza katika Jarida la Kemia na Madawa la nchini Marekani,
mwaka 2010.
Taasisi ya utafiti wa Saratani ya Nchini Uingereza(NIR) ilifanya utafiti wa kwanza kuhusu maajabu ya stafeli mwaka 1976. Katika
utafiti huo ilibainika kuwa majani, mizizi na tunda la stafeli, vina
uwezo wa kutibu saratani, lakini matokeo ya utafiti huo hayakutangazwa
kwa umma kwa hofu ya kuua viwanda vya dawa za saratani.
Inaelezwa
kuwa kirutubisho kilichopo katika stafeli kinatumia jina la kibiashara
la ‘Triamazon’ na kimepigwa marufuku kutumika nchini Uingereza na
Marekani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kitiba.Utafiti
mwingine uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kikatoliki nchini Korea na
kuchapishwa katika jarida la Bidhaa Asilia ulibaini kuwa stafeli lina
uwezo wa kuponya saratani ya tumbo.
Utafiti
wa chuo hicho ulienda mbali na kusema kuwa tunda hilo linaweza kulenga
seli za saratani tu, bila kushambulia seli muhimu za mwili kama ambavyo
tiba ya mionzi ifanyavyo.
Tunda la
Stafeli lina kirutubisho muhimu kiitwacho Annona Muricata, ambacho
ndicho chenye uwezo wa kupigana na maradhi ya saratani. Imeelezwa kuwa stafeli lina uwezo wa kutibu aina 12 za saratani ikiwemo ya matiti, kongosho, mapafu na ya kibofu cha mkojo.
Pamoja na
kutibu saratani, kirutubisho hicho kilichopo katika tunda hilo pia
huweza kutibu vimelea, shinikizo la damu, msongo wa mawazo, matatizo ya
mfumo wa fahamu na sukari.Utafiti
huo unaonyesha kuwa kirutubisho kimegwacho katika tunda hilo kinaweza
kwa asilimia kubwa kupambana na saratani bila kumuacha mgonjwa na
madhara kama kusikia kichefuchefu, kutapika, kupungua uzito na
kunyonyoka nywele.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog