Katibu
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashilila
akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu ukiukwaji wa kanuni za
bunge uliofanywa na baadhi ya wabunge wakati wa mkutano wa 10 wa
bunge uliomalizika mjini Dodoma na mabadiliko yaliyofanyika kwa baadhi
ya kamati kuondolewa pamoja na uundwaji wa kamati mpya 3
zitakazoshughulikia Ushirikiano wa Afrika, Mashariki, Bajeti, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa. (Picha na Aron Msigwa)
Katibu
wa Bunge Dk Thomas Kashilila akizungumza na Wanahabari jijini Dar es
Salaam leo wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya
bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge amesema Bunge
linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja
(LIVE) kupitia televisheni kwa nia ya kukomesha vitendo vya baadhi ya
Wabunge wanaokikuka kwa makusudi Kanuni za Bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila na hivyo kutoa picha mbaya katika jamii.
Akasema ili kurejeza maadili kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.
Akasema jamii imeendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi kutokana na kukiukwa kanuni hizo.
Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.
Ameahidi kuwa ofisi yake itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika utoaji wa taarifa mbalimbali za bunge pamoja na uandaaji wa mafunzo ya mara kwa mara kwa waandishi wanaoandika habari za bunge, huku akiwasisitiza waandishi wa habari kuitumia ipasavyo ofisi yake kupata taarifa sahihi za kuwasaidia katika uandishi.

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog