Facebook Comments Box

Wednesday, September 5, 2012

EWURA YAPANDISHA TENA BEI YA MAFUTA


Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini ambapo bei ya petroli na mafuta ya taa zimepanda. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo jana bei mpya zitaanza kutumika kuanzia leo.
Sambamba na kupanda kwa gharama halisi za uagizaji wa mafuta kutoka kwenye soko la Dunia, bei za jumla na rejareja kwa mafuta aina zote zimebadilika ikilinganishwa na taarifa iliyopita ya Agosti 1, 2012.
Petroli imeongezeka kwa sh 291 kwa lita sawa na asilimia 14.50 Dizeli imeongezeka kwa Sh 199 kwa lita sawa na asilimia 10.26 na mafuta ya Taa Sh 67 kwa lita sawa na asilimia 3.63
Ameeleza kuwa kampuni zipo huru kuweka bei inayotaka kulingana na ushindani ilimradi isivuke bei elekeze ya mamlaka hiyo (EWURA)

Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU