Facebook Comments Box

Tuesday, August 28, 2012

CHADEMA YASEMA POLISI HAIWEZI KUKWEPA LAWAMA YA MAUAJI

Chadema imesema kuwa polisi haiwezi kukwepa lawama juu ya kifo cha kijana Ally Zona mwenye umri wa miaka 38 kilichotokea huko Morogoro. Vilevile CHADEMA kimesitisha maandamano katika Mkoa wa Iringa kupisha zoezi la sensa. akizungumza na waaandishi wa habari katibu mkuu wa cha hicho Dr. Slaa amesema baada ya zoezi hilo kuisha wataendelea na maandamano na kampeni yao maarufu kwa jina la Movement for Change (M4C). Wakati huhuo chama cha chadema kimesema kitagharamia mazishi ya kijana huyo aliefariki huku ikisubiri ripoti kutoka kwa Daktari na mwanasheria wao ili kujua hatua gani ya kuchukua

Katibu mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa akiongea na waandishi kwenye hoteli ya Mount Uluguru




Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU