Facebook Comments Box

Wednesday, August 3, 2016

TETESI ZA USAJILI ULAYA


Chelsea wako tayari kumtoa mshambuliaji wa Ufaransa Loic Remy, 29, pamoja na dau litakaloweka rekodi Uingereza kitita cha paundi millioni 65 kwa mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, 23. (Chanzo Daily Mail)

Everton wamekuwa waking’ang’ania wapewe paundi millioni 75 kwa mchezaji huyo pekee ambaye walimsajili kutoka Chelsea kwa paundi millioni 28 miaka miwili iliyopita. (Chanzo Sun)

Lukaku anafikiria kutoa ombi rasmi ili kulazimisha arudi tena Stamford Bridge. (Chanzo London Evening Standard)

Winga wa Leicester City Riyad Mahrez, 25, amekubali kuhamia Arsenal, hii ni kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka nchini Algeria. (Chanzo Le Buteur)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kufikia muafaka juu ya dili la paundi millioni 50 la uhamisho wa beki John Stones, ambaye ndiye lengo lake kuu, ingawa Everton wamesisitiza kuwa bado kuna 'gepu kubwa' kati ya klabu hizo mbili juu ya ada ya uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Chanzo Daily Mirror)

Real Madrid inaweza ikawapa ofa Newcastle ya wachezaji wawili vijana - pengine Mariano Diaz, 23, na Marcos Llorente, 21 – kwa mikopo wa muda mrefu ikiwa ni kama sehemu ya mpango wa kumchukua kiungo wa Ufaransa Moussa Sissoko, 26. (Chanzo Guardian)

Stoke City wanafikiria kumtoa aidha Joselu, 26, Mame Diouf, 28, au Peter Crouch, 35, ikiwa West Bromwich Albion watataka wapewe mchezaji wa kubadilishana kwenye dili la uhamisho wa Saido Berahino, 22. (Chanzo Stoke Sentinel)

Paris St-Germain wamekubali kuwalipa Real Madrid yuro millioni 25 kama ada ya kumsajili winga Jese Rodriguez, 23. (Chanzo Marca)

Bastian Schweinsteiger ameambiwa atapewa nafasi ya kurudi Bayern Munich ikiwa ataondoka Manchester United. (Chanzo Sky Sports)



Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU