Serikali ya China na wataalamu wake kadhaa wanasema matumizi ya windows 8 ni hatari kwa usalama wao na ustawi wao , kwahiyo wamekataza na kuendelea kutengeneza program yao ya COS (China Operating System) kwa ajili ya matumizi ya serikali pamoja na taasisi zake .
Suala kama hili liliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita huko ulaya , lakini umoja wa ulaya ulienda mahakamani na mahakama ikaamua Microsoft itoe source code kwa umoja wa ulaya ili waweze kubadilisha na kuweka mambo yao kwa maslahi ya umoja wa ulaya
Kitu kikubwa ambacho serikali ya uchina inalalamikia kuhusu Windows 8 ni hii source code, serikali ya china inataka source code ya bidhaa hii ili iweze kuifanyia mabadiliko iendane na maslahi yake haswa kwenye mambo ya ulinzi na usalama .
Hapa nchini kwetu tumeona taasisi mbalimbali na wizara mbalimbali za serikali tena nyeti zikitumia bidhaa mbalimbali za windows bila kufanya mabadiliko yoyote kwa ajili ya usalama wao , tumeona watu haswa viongozi wakinunua kompyuta na vifaa vingine vya mawasilino na kuvitumia kuhifadhi taarifa nyeti bila vifaa hivi kuchunguzwa au kubadilishwa chochote.
Wakati serikali inafikiria kupeleka muswada wa sheria ya usalama wa mtandao bungeni , ni vizuri suala kama hili lijulikana na wataalamu watakaojadili sera au chochote kinachohusiana na usalama wa Taifa .Huwezi kulinda taifa kama taarifa zako zinaweza kuchukuliwa au kuangaliwa na mtu akiwa popote duniani .
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog