Facebook Comments Box

Wednesday, June 12, 2013

AMPIGA MUMEWE BAADA YA KUKUTA AKIANGALIA TV KABLA YA KUMALIZA KAZI ZA NYUMBANI

MWANAMUME mmoja katika mtaa wa Mwanzo, Eldoret anauguza majeraha baada ya kupigwa na mkewe kufuatia mzozo uliotokana na yeye kupatikana akitazama runinga kabla ya kumaliza kazi ya nyumbani.

Kwa mujibu wa majirani mkewe mwanamume huyo, alirejea nyumbani jioni kutoka kazini mnamo Jumatatu na kumkuta akitazama televisheni. Mara moja, alimrukia na kumpiga vibaya.

Mwanaume huyo aliokolewa na majirani waliofika kuitika kilio chake na kumkuta akigaragara sebuleni kutokana na maumivu. Walimpeleka katika zahanati ya kibinafsi alikotibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani.

Majirani walisema wawili hao wamekuwa wakigombana mara kwa mara baada ya mwanamume huyo
kufutwa kazi miezi michache iliyopita.

Wakazi wa Mwanzo sasa wanalitaka Shirika la Maendeleo ya Wanaume kuingilia kati na kuokoa wanaume ambao wanadai wanadhulumiwa na kuchapwa na wake zao kila siku. Wanasema visa hivyo vimeongezeka mtaani humo. Aidha, wanataka wanaume hao wapewe ushauri wa kisheria kuwasaidia kutafuta usaidizi.

Mmoja wa wakazi, Justus Mwaniki, alisema wanaume wengi wanapigwa na wake zao kwa kuonekana kama mzigo nyumbani hasa wanapokosa kazi: “Sisi huwatunza wake zetu, na kukidhi mahitaji hao hata wakiwa hawana kazi na huleta nyumbani mapato yetu kwa matumizi ya familia. Mbona wadhulumu wanaume ambao hawana kazi?” alishangaa.

Majuzi, kiongozi wa Maendeleo ya Wanaume Nderitu Njoka alijipata taabani baada ya kukaripiwa na mwanamke mwenye nyumba kaunti ya Kiambu alipokuwa ameenda kumwoka mwanamume aliyedai alikuwa akizuiliwa na kudhulumiwa nyumbani.


Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog
 

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU