
Katika mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa jana (Aprili 
14 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000 
kutokana na watazamaji 11,458.
Viingilio
 katika mechi hiyo iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 
mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku 
kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la
 Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34.
Mgawo
 mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, 
tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi 
sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 
2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) 
sh. 1,849,326.14.
WATAZAMAJI 11,021 WAZISHUHUDIA YANGA, OLJORO
Watazamaji
 11,021 walikata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya 
Yanga na Oljoro JKT iliyochezwa juzi (Aprili 13 mwaka huu) Uwanja wa 
Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 63,170,000.
Viingilio
 katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi 
wa mabao 3-0 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 
huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 14,853,252.45 wakati Kodi ya 
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 9,636,101.69.
Mgawo
 mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,552,501.25, 
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,531,500.75, Kamati ya Ligi 
sh. 4,531,500.75, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 
2,265,750.37 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) 
sh. 1,762,250.29.
Facebook Comments Plugin Enhanced by Kitongoni blog